• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

DCEA:Raia wa nchi jirani wanafadhili kilimo cha bangi Mara,yakamata tani 7.8

Yatoa miezi mitatu wananchi kuacha kujihusisha nacho,yafyeka ekari zaidi ya 3000

by bajeti
October 9, 2024
in Habari
0
DCEA:Raia wa nchi jirani wanafadhili kilimo cha bangi Mara,yakamata tani 7.8
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MARA

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi pamoja  na wananchi imefanya operesheni kubwa ya kihistoria wilayani Tarime na Serengeti,Mkoa wa Mara kukabiliana na tatizo la uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya, hususani bangi.

Operesheni hiyo iliyoshirikisha Jeshi la Polisi na Jeshi la Akiba(Mgambo) imefanyika kwa muda wa wiki tatu katika wilaya hizo kwenye vijiji vya  Matongo, Nyarwana, na Weigita vilivyopo Bonde la Masinki.

Mbali na vijiji hivyo lakini pia imehusisha  pia vijiji vya  Nkerege, Kembwe, Nyakunguru na Iseresere pamoja na eneo la Bonde la Mto Mara.

Akizungumza mara baada ya operesheni hiyo Oktoba 8, 2024 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)Aretas Lyimo amesema, jumla ya ekari 3,007.5 za mashamba ya  bangi  zimeteketezwa katika operesheni hiyo.

Aidha amefafanuwa kuwa kilogramu 7,832.5  za bangi kavu, na kilogramu 452 za mbegu za bangi  zimekamatwa, ambapo watuhumiwa 17 pia  wamekamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani.

Kamishna JeneraliLyimo amesema operesheni hii ni sehemu ya jitihada za serikali kulinda jamii dhidi ya madhara ya dawa za kulevya na amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kutoa taarifa kuhusu shughuli zinazohusiana na dawa hizo.

Kamishna Jenerali Lyimo amefafanuwa kuwa Mamlaka imebaini kilimo cha bangi mkoani Mara kinafadhiliwa na raia wa nchi jirani ambao huwapa mitaji wakulima wa Tarime kisha bangi ikishakomaa huvunwa na kusafirishwa kwenda  kuuzwa.

“Tunatoa miezi mitatu kwa wananchi wa Mkoa wa Mara kuhakikisha wanaacha kabisa kujihusisha na kilimo cha bangi.

‘’Baada ya muda huo, tutafanya operesheni kubwa kwa namna nyingine na kuhakikisha maeneo haya yanabadilishiwa matumizi na hayatumiki tena kwa kilimo cha  bangi.

‘’Pia wote wanaotetea uhalifu huu watachukuliwa hatua ili kuhakikisha wananchi wote wanatii sheria za nchi”amebainisha Kamishna Jenerali Lyimo

Wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wakishiriki operesheni ya kutokomeza dawa za kulevya aina ya bangi iliyoendeshwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dwa za Kulevya (DCEA) hivi karibuni(Picha na DCEA)

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amekiri wilaya yake kukabiliwa na changamoto ya kilimo cha bangi hususani katika eneo la Bonde la Mto Mara na tayari serikali imeanza kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto hiyo.

“Tumeanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya bangi na hasara wanayoweza kuipata kwa kujihusisha na kilimo cha bangi na walio wengi wametuahidi kuachana na kilimo cha bangi”amebainisha Meja Gowele

Kwa upande wake Afisa wa Maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Dakio la Mara Mwita Mataro amesema lengo kubwa la bodi ni kuhakikisha rasilimali za maji zinatunzwa na kuendelezwa pasipo kuruhusu uharibifu wa aina yoyote.

“Tumejionea hali halisi ya bonde na tumeshuhudia zao la bangi likiwa limelimwa katika Bonde la mto Mara”amesema Mataro

Mataro amefafanuwa kuwa sheria za rasilimali za maji haziruhusu kilimo haramu cha zao la bangi hata mazao mengine halali yanapaswa kulimwa umbali wa mita 60 kutoka mtoni.

‘’Hao wanaolima bangi ni sehemu ya watu wanaoharibu vyanzo vya maji kwa sababu mwisho wa siku huu udongo wote mvua zitakaponyesha tope lote linatiririkka kwenda kwenye mto’’ ameongeza Mataro.

Mataro ambaye pia ni msimamizi wa Rasilimali za Maji katika Mkoa wa Mara amesema Bodi hiyo imeandaa mpango kwa kidakio cha Kaskazini ambao unataja shughuli gani zinatakiwa kufanyika kwenye vyanzo vya maji ambazo ni rafiki, na wao kama bodi watasimamia kuhakikisha mipango hiyo inatekelezwa na hifadhi ya maji inalindwa.

Shamba la bangi Tarime mkoani Mara

Naye Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Lepapa Molel amebainisha kuwa wakulima wengi wanalima bangi kwa kutegemea maji yanayotoka Mto Mara

“Nashauri wakulima wageuke na kuanza kulima mazao ya chakula yanayoweza kuwapa chakula na fedha  kuliko bangi”ameeleza Molel 

 

Next Post
Operesheni ya DCEA yasaidia wanakijiji kukataa kilimo cha bangi Tarime

Operesheni ya DCEA yasaidia wanakijiji kukataa kilimo cha bangi Tarime

RC Sendiga ataka uhamasishaji usajili wakulima wanufaike na mbolea za ruzuku

RC Sendiga ataka uhamasishaji usajili wakulima wanufaike na mbolea za ruzuku

IGP Wambura atua Tabora kuangalia hali ya usalama

IGP Wambura atua Tabora kuangalia hali ya usalama

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In