• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Dkt.Mpango ataka matumizi ya ndoo kama choo magerezani kuondolewa

Ataka kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai

by bajeti
October 25, 2024
in Mazingira
0
Dkt.Mpango ataka matumizi ya ndoo kama choo magerezani kuondolewa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikagua Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, Msalato mkoani Dodoma kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza. Oktoba 24,2024.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Magereza kuondoa kabisa matumizi ya ndoo magerezani kama choo ikiwemo kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki Jinai pamoja na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuboresha huduma za urekebu na ufanisi wa Jeshi hilo.

Amesema pia taarifa ya Tume ya Haki Jinai ilianisha utumiaji wa nguvu kupita kiasi ikiwa ni pamoja na ukaguzi unaotweza utu na kukiuka haki za binadamu ikiwemo Viongozi na Maafisa Magereza kubadili mtazamo ili kuendana na mazingira ya sasa

Makamu wa Rais ameyasema hayo Oktoba 24,2024 wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza unaofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Msalato mkoani Dodoma.

Amesema ni muhimu kwa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Magereza kuchukua hatua zinazowezekana kwa kutumia rasiliamli zilizopo, kuondoa dhana ya kudhalilisha utu na kukiuka haki za binadamu.

”Ni muhimu  kupunguza na hatimaye kuondokana kabisa na matumizi ya ndoo magerezani kama choo”amesema Dkt.Mpango

Aidha ameomba kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya juhudi kuwapatia wafungwa vifaa vitakavyowasaidia kujiendeleza kielimu wanapokuwa magerezani kama kompyuta, vitabu na vifaa vingine.

Amesema kinachohitajika zaidi ni dhamiri ya dhati na ubunifu ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za urekebu na kupunguza idadi ya wanaomaliza vifungo vyao kurejea tena magerezani.

Aidha ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Magereza unakamilika mapema na unazingatia mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai na hali ya sasa.

Dkt.Mpango amesisitiza umuhimu wa  Jeshi la Magereza kushirikiana  na Jeshi la Polisi pamoja na Bodi ya Parole kuweka utaratibu wa kuwatambua na kuwafuatilia wale wanaotoka Magerezani kwa msamaha na hata wale waliomaliza vifungo vyao wanakokwenda na jinsi wanavyoenenda.

Amebainisha kuwa taarifa zimeainisha mambo mbalimbali  yanayoplekea  wafungwa wanaomaliza vifungo vyao kufungwa tena kuwa ni pamoja na kukosekana kwa miongozo rasmi ya magereza ya namna ya kutekeleza programu za urekebu, kutokuwepo na utaratibu mzuri wa kubaini na kuwatenga wafungwa kwa ajili ya programu za urekebu kulingana na vipaji vyao, kutokuwepo kwa programu za kutosha za huduma za kielimu na kisaikolojia kwa wafungwa pamoja na kukosekana kwa programu za kuwaandaa wafungwa wanaokaribia kumaliza vifungo.

Aidha ameongeza kuwa ni muhimu kwa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula na kuimarisha usimamizi wa miradi inayoendeshwa na Jeshi hilo na kulitaka kuweke nguvu katika kuzalisha miche na mbegu hususan za mazao ya kimkakati ili kulisaidia Taifa kuondokana na utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi.

Dkt.Mpango ameeleza kuwa ni muhimu Jeshi la Magereza kujizatiti katika sekta ya ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali kwa ajili ya matumizi magerezani na kuuza ziada katika soko la ndani na nje ya nchi na kuongeza jitihada katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi ya kupikia.

‘’Ni muhimu wa kila gereza kutunza msitu wa asili ulio karibu au kuanzisha msitu wa kielelezo kwa kupanda miti, kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo na kuwataka uongozi wa wilaya na mkoa kusaidia kufanikisha kazi hiyo.amesema Dkt.Mpango

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu amesema Jeshi hilo limeendelea kuimarisha matumizi ya Mahakama mtandao katika magereza ambapo kufikia sasa jumla ya magereza 66 yana huduma hizo zinazosaidia wahalifu kuweza kusikiliza mashauri yao wakiwa magerezani.

Aidha amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 zimetengwa jumla ya Sh.Bilioni 1.3 kwa ajili ya kujenga vyumba vya mahakama mtandao katika magereza 20 yaliyopo nchini ikiwemo kiasi cha Sh.Milioni 451.5 zilizotengwa kwa ajili ya kuweka mfumo wa taarifa za wahalifu.

CGP Katungu amebainisha kuwa katika jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama magerezani, Jeshi hilo limefunga mfumo wa CCTV katika magereza 10 ambapo inatarajiwa kuendelea kuweka huduma hiyo katika magereza yote nchini.

 

 

Next Post
BRELA yatekeleza agizo la Rais Dkt.Samia kuhusu Mifumo ya Kitaasisi kusomana

BRELA yatekeleza agizo la Rais Dkt.Samia kuhusu Mifumo ya Kitaasisi kusomana

TARI,ZARI na NIBIO wajadili  Afya ya Udongo

TARI,ZARI na NIBIO wajadili Afya ya Udongo

Serikali yapeleka mamilioni ya fedha kuimarisha kitengo cha maabara na mifupa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara

Serikali yapeleka mamilioni ya fedha kuimarisha kitengo cha maabara na mifupa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In