• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tanzania,Uingereza kushirikiana kuendeleza Sekta ya Madini

Taasisi za Jiolojia na Utafiti Madini za Tanzania na Uingereza kushirikiana

by bajeti
January 9, 2025
in Mazingira
0
Tanzania,Uingereza kushirikiana kuendeleza  Sekta ya Madini

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marriane Young Januari 8,2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya balozi huyo kumtembelea ofisini kwake.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye Sekta ya Madini hususani katika kujengea uwezo watu wake, kubadilishana uzoefu na  uongezaji thamani madini

Mbali na hilo lakini pia kuwekeza kwenye kufanya tafiti mbalimbali ili kukuza sekta hiyo na kupanua mnyororo wa thamani utakaoongeza ajira na kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa.

Hayo, yameelezwa Januari 8.2025 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde katika Ofisi ndogo za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Marianne Young.

Mavunde amesema  Balozi Young amefika ofisini kujitambulisha kwa kuwa ana muda mfupi nchini tangu awasili na wamezungumzia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Uingereza.

Ameongeza kuwa  Tanzania na Uingereza zimekubaliana katika kuwajengea uwezo watu wake na kubadilishana uzoefu hususani katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini (GST) na British Geological Survey (BGS)ya Uingereza ili kuwajengea uwezo Watanzania kwa kuwa na ujuzi stahiki katika masuala ya uendelezaji wa Sekta ya Madini

‘’Eneo la pili tulilozungumzia kwa urefu ni katika madini,mkakati ambapo Uingereza wameonesha utayari katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini,mkakati ambapo Tanzania imejipanga kuhakikisha inavutia uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hapa nchini.

‘’Sasa ni muda muafaka wa kuhakikisha madini ya kimkakati yanawanufaisha Watanzania na Taifa, na ndiyo maana tumeandaa mkakati maalum wa kutekeleza azma hiyo huku ikizingatiwa kuwa madini hayo kwa sasa yana mahitaji makubwa duniani.

‘’Tupo katika hatua za mwisho kukamilisha mkakati huu maalum wa madini na muhimu ambao pia ni sehemu ya Kampeni ya Dunia katika kupunguza hewa ya ukaa kupitia matumizi ya nishati safi,” amesema Mavunde.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marriane Young Januari 8,2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya balozi huyo kumtembelea ofisini kwake.

Akizungumza katika Mkutano huo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania  Marriane Young amesema Uingereza inapongeza jitihada kubwa za kukuza Sekta ya Madini zinazofanywa na Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuahidi kuimarisha ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizi hasa katika kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo kupitia Taasisi za madini nchini Uingereza na Tanzania.

Balozi Young ameunga mkono mpango wa uongezaji thamani madini nchini na kuahidi kwamba Uingereza itashirikiana na Tanzania kwa ukaribu ili malengo hayo ya timie.

Next Post
Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In