• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, December 5, 2025
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Mhandisi Lwamo ataka udhibiti kuepusha maafa

by bajeti
January 15, 2025
in Mazingira
0
Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo  (katikati) akisikiliza mada wakati wa kikao na wakaguzi migodi na baruti (hawapo pichani) kilichofanyika Januari 13,2024 jijini Dodoma na kusisitiza umuhimu wa udhibiti wa bariti ili kuepusha maafa.(Picha na Tume ya Madini)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MATUMIZI ya Baruti  nchini yameongezeka kutoka  tani 3,000 kwa  mwaka katika miaka ya 1990 hadi kufikia wastani wa tani 26,516.07 kwa mwaka 2024.

Mbali na hilo lakini pia hadi sasa kuna zaidi ya bohari (magazine) 231, stoo 493, masanduku ya kuhifadhia baruti zaidi ya 279 yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutunzia baruti migodini na maeneo ya biashara ya baruti.

Takwimu hizo zimetolewa Januari 13, 2025 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo  wakati akifungua kikao cha kuwajengea uwezo  wakaguzi migodi na baruti.

Amesema, kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini, utafiti wa mafuta na gesi asilia na ujenzi wa miundombinu mbalimbali, kuongezeka kwa matumizi hayo pia kumepelekea kupanuka kwa biashara ya baruti hapa nchini.

“Matumizi makubwa ya baruti maana yake uchimbaji umeongezeka, hivyo bila udhibiti italeta madhara, kikao hiki ni kujengeana uwezo na lengo ni kuhakikisha wachimbaji hawapotezi maisha au kupoteza viungo kwa ajili ya matumizi ya baruti.

“Ongezeko la uhitaji wa matumizi ya baruti hapa nchini kumepelekea uwepo wa changamoto kadhaa katika usimamizi wake, udhibiti madhubuti ni muhimu, mkadhibiti katika maeneo yenu, itakuwa ni aibu mkaguzi mgodi na baruti eneo lake mtu akapata madhara,”amesema Mhandisi Lwamo .

Mhandisi Lwamo amebainisha kuwa,mpaka sasa kuna zaidi ya bohari (magazine) 231, stoo 493, masanduku ya kuhifadhia baruti zaidi ya 279 yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutunzia baruti migodini na maeneo ya biashara ya baruti.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na   wakaguzi migodi na baruti mara baada ya kikao cha kuwajengea uwezo wakaguzi hao kilichofanyika Januari 13,2024 jijini Dodoma(Picha na Tume ya Madini)

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira, Hamisi Kamando amesema kumekuwa na matukio mbalimbali ya ajali yanayotokana na kutokuzingatiwa kwa Sheria ya Baruti ya Mwaka 1963, Kanuni za Baruti za Mwaka 1964 na taratibu zingine katika usimamizi wa Baruti.

Naye, Mwanasheria kutoka Tume ya Madini  Damian Kaseko amewataka wakaguzi migodi na baruti kusimamia Sheria, Kanuni na Sera wanapotekeleza majukumu yao ili kuepusha migogoro na kuwa na mipaka katika utekelezaji wa shughuli zao.

Next Post
Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

DCEA yateketeza ekari 157 za bangi Kondoa

DCEA yateketeza ekari 157 za bangi Kondoa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:25
  • Today's page views 25
  • Total visitors 12,066
  • Total page views 13,719

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In