NA MWANDISHI WETU,DODOMA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Spika Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, kilichotokea Agosti 06, 2025 Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agost 6,2025 na Kitengo cha Mawasilianona Elimu kwa Umma cha Ofisi ya Bunge Agosti 6,2025 jijini Dodoma na kuwekwa pia katika tuvuti ya Bunge imeeleza kuwa marehemu Ndugai amefariki leoAgosti 6,2025 jijini Dodoma
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma.
Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.




Discussion about this post