• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Michezo

Adaiwa kumuua mwenzie kisa ushabiki wa timu za Simba na Yanga

by bajeti
September 17, 2025
in Michezo
0
Ajali iliyohusisha Bajaji yauwa watu watano Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP- Augustino Senga

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,SONGWE

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na msako wa kumtafuta Exavery Mwaweza kwa tuhuma za kumjeruhi na kusababisha kifo cha Evaristo Mwambogolo mkazi wa Wilaya na Mbozi

Mwaweza anadaiwa kumchoma kisu kifuani Mwambogolo baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni ya mabishano ya mpira wa miguu kati ya  timu za Simba na Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 17,2025 kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga amesema tukio la mauaji hayo lilitokea mnamo Septemba 16,2025 saa 12:50 jioni katika Kitongoji cha Ululu,Kijiji na Kata ya Idiwili wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe

Amesema katika tukio hilo,Evaristo Mwambogolo mkazi wa Ululu wilayani Mbozi alichomwa kisu kifuani,eneo la moyo  na mtu aliyefahamika kwa jina la Exavery Mwaweza baada ya mabishani ya mpira wa miguu kati ya timu za Simba na Yanga

“Marehemu alijeruhiwa vibaya na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa kwenye Zahanati ya Iyula iliyopo Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya  matibabu.

“Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ushabiki wa mpira wa timu ya Simba na Yanga kati ya marehemu na mtuhumiwa,ambapo mtuhumiwa alitumia kisi alichokuwa nacho wakati wa ugomvi huo na mara baada ya kutenda kosa hilo alitoroka kusikojulikana”amesema Kamanda Senga

Kamanda Senga amebainisha kjuwa Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili akamatwe na aweze kuhukumiwa kwa mujibu wa sharia

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi,na kutojihusisha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na upotevu wa maisha.

“Jeshi la Polisi linawataka wananachi kuendelea kudumisha amani,mshikamano na utulivu,hasa wakati wa mijadala au mabishano ya kawaida ikiwemo michezo”ameongeza Kamanda Senga

Next Post
Makamu wa Rais Dkt.Mpango azungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Japan

Makamu wa Rais Dkt.Mpango azungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Japan

Serikali ya ADA-TADEA kuwalipa askari walioshiriki vita vya Kagera

Serikali ya ADA-TADEA kuwalipa askari walioshiriki vita vya Kagera

Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

CCM kuwezesha ujenzi wa  nyumba 50,000 za makazi ya bei nafuu ifikapo 2030

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In