• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

IGP Wambura:Sasa hivi si muda wa kuuziana mbuzi kwenye gunia

Asema mambo yote yako hadharani,kununua ndege mbili mpya.

by bajeti
May 29, 2026
in Habari
0
IGP Wambura:Sasa hivi si muda wa kuuziana mbuzi kwenye gunia

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Camillius Wambura

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillius Wambura ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kulipatia Jeshi hilo mahitaji muhimu  ya kimuundo na kimfumo na kuongeza kuwa huu sio wakati wa kuuziwa mbuzi kwenye gunia.

IGP Wambura amesema Serikali imelipatia fedha Jeshi hilo mbali na kununua vifaa kama magari lakini pia kujenga majengo ya  makazi ya askari ambao walikuwa wakiishi katika nyumba kama za wavuvi jijini Dodoma ambapo pia kwa sasa wako katika hatua za kununua ndege mbili mpya ili kuboresha utendaji kazi wa Jeshi hilo.

IGP Wambura ameyasema hayo Mei 28,2026 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Dar es Salaam katika hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi zaidi ya 700 katika Chuo cha Taaluma cha jeshi hilo kilichopo barabara ya Kilwa.

Amesema Jeshi la Polisi limewezeshwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za muda mrefu za ufinyu wa bajeti,miundombinu mbalimbali pamoja na vitendea kazi.

Amesema kwa upande wa majengo,Jeshi la Polisi limetekeleza jumla ya miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo 320 ambapo limefanikiwa kukamilisha majengo 174 na kuendeleza miradi ya ujenzi na ukarabati wa majengo 146 ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

“Miradi hii kwa ufupi Mheshimiwa Rais ni kama ifuatavyo,Ofisi za Makamanda wa Mikoa 18,kati ya hiyo majengo 10 yapo katika hatua mbalimbali na hatua za mwisho za ujenzi,Vituo vya Polisi Daraja A  15 kati ya hivyo vituo saba vinamalizikia kujengwa.

“Vituo vya Polisi Daraja B  na ujenzi wa ukarabati wa makazi ya askari 139 na 46 kati ya hayo yapo kwenye hatua za mwisho,aidha  tunaendelea na ujenzi pamoja na ukarabati wa majengo ya matumizi mengine ya Jeshi la Polisi ambapo jumla ya miradi 46 imetekelezwa na kati ya hiyo miradi 33 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji”amesema IGP Wambura

Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi wakila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) Mei 28,2026 mkoani Dar es Salaam wakati wa kuhitimu katika Chuo cha Taaluma cha Jeshi hilo kilichopo barabara ya Kilwa.

Aidha amesema miradi hiyo inahusisha ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro na ujenzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi mkoani Kilimanjaro.

IGP Wambura ameyataja majengo kuwa ni  Rest House,Jengo la Hospitali ya Rufaa Kilwa Road,Vituo Tiba vya Polisi katika baadhi ya mikoa ,Karakana ya TEHAMA  na majengo ya vikosi mbalimbali vya Polisi.

“Mheshimiwa Rais jambo la kujivunia zaidi ni kwamba majengo haya yaliyokamilika pamoja na yale yanayoendelea  kutekelezwa yanasimamiwa na kutekelezwa kupitia Kikosi cha Polisi cha Ujenzi”amesema IGP Wambura

IGP Wambura ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lina wataalam wa kada mbalimbali za ujenzi wakiwemo Wasanifu Majengo,Wakadiriaji Majenzi pamoja na wahandisi wa fani tofauti za ujenzi ambao kwa pamoja wameendelea kufanya kazi kubwa kwa weledi na uzalendo mkubwa ambapo hali hii imeendelea kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi.

“Mheshimiwa Rais naomba nitumie jakwaa hili kuelezea jambo hili kubwa,haya ni majengo yaliyojengwa si kwa miaka mitano ya uongozi wako ni ndani ya miaka mitatu,lakini wakati majengo haya yanaendelea utaona ni hali gani uliikuta.

“Lakini kuna majengo mengine sijui makazi ya Dodoma yataonekana hapo yalikuwa ni makazi ya askari pale Dodoma.

“Utakapoona Mheshimiwa Rais  ile si kambi ya wavuvi,hayo ndiyo makazi ya askari polisi uliyoyakuta,hayo hapo si kambi ya wavuvi,askari walilala humo,waliamka humo na walikwenda kutimiza na kutekeleza wajibu wao wa kulinda watu na usalama wao”amebainisha IGP Wambura

Aidha ameeleza kuwa makazi hayo yamekuwepo hapo kwa muda wa miaka mingi sana na Rais Dkt.Samia ameyakataa na sasa ametoa fedha na kuhakikisha kunajengwa majengo mazuri ya makazi ya askari ya maghorofa yenye sakafu nne kila moja.

“Haya ndio yameondoa yale makazi ambayo kwa hakika hata wavuvi walikuwa hawaishi mle,Mheshimiwa Rais umekataa,haya ndio majengo tunayomiliki sasa Jeshi la Polisi.

“Tutaacha vibanda viwili kama kumbukumbu kwamba Jeshi hili liliwahi kupita katika kadhia hii lakini kwa sasa alikuwepo au alikuja Rais fulani anayeitwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akatutoa mle ndani akatuweka kwenye majengo haya.

“Sisi ni akina nani tusisimulie hadithi hii,nzuri,sisi tusiokuwa na roho ya shukurani ambao hatuwezi kusimulia hadithi hii nzuri tutakuwa ni binadamu gani”ameongeza IGP Wambura

IGP Wambura amemshukuru Rais Dkt.Samia  na kuomba Mungu aendelee kumbariki na kumsimamia na kumpa afya njema.

Kwa upande wa vyombo vya moto na usafiri,IGP Wambura amebainisha kuwa Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imewawezesha kupata vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari 1394 ya kioparesheni na matumizi mengine kwa kipindi kifupi kisichozidi miaka mitatu.

“Hapo unapoona,hapo sio bandarini,hii ni yadi yetu ya Polisi ya kupokelea magari na hayo yote ni magari mapya ,mazuri na ya kisasa na ndio yanayosababisha tunafanya kazi bila mkwamo wa aina yoyote.

“Magari haya yamekuja kuchukua nafasi ya magari mabovu tuliokuwa nayo,Mheshimiwa Rais nimewahi kuona Afisa wa Polisi akienda ofisini na gari alilopanda inasukumwa kuanzia nyumbani kwake hadi anafika ofisini na baadaye jioni,haijawaka inasukumwa tena kutoka ofisini mpaka inafika nyumbani hiyo gari hajawaka.

“Haya yote yamekuja kuondolewa na wewe mheshimiwa Rais,magari 1394 kwa kipindi cha miaka mitatu,kwa kipindi hicho tumeweza kupata pikipiki 39 za kuongoza misafara na pikipiki 105 za doria,boti 13 za doria na kufanya matengenezo ya ndege moja na sasa tuko kwenye mchakato wa kununua ndege mpya mbili”amefafanuwa IGP Wambura

Aidha IGP Wambura ameeleza kuwa hapo bado hajagusia uwezeshwaji mkubwa uliofanywa katika maeneo mengine muhimu kama maslahi,ajira,mashine za kisasa za ushonaji,sare,silaha vifaa vya uchunguzi wa kisayansi na upelelezi,vifaa vya muziki,mashine za kisasa za uchapaji pamoja na vifaa mbalimbali vya kioparesheni.

“Mambo haya yote yanapaswa kusemwa ukiwepo ili watanzania waendelee kuona na kuelewa dhamira yako ambayo imekuwa ikienda sambamba na vitendo.

“Tarehe 22 Mwezi Mei 2026 pale Shule ya Polisi Tanzania-Moshi nilitoa jumla ya wanafunzi 5514,hawa ni wanafunzi wa kozi ya awali waliohitimu mafunzo katika shule hiyo na kuwa askari wa Jeshi la Polisi”amesema IGP Wambura

IGP Wambura amebainisha kuwa miongoni mwa vijana hao,wapo waliotoka katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na familia zenye hali ngumu ya kiuchumi lakini wenye sifa na ufaulu uliowawezesha kupata nafasi hiyo.

Ameongeza kuwa hiyo ni sehemu ya dhamira ya Serikali yake ya kuhakikisha kuwa fursa ndani ya Jeshi la Polisi zinawafikia watanzania wa makundi mbalimbali bila ubaguzi huku wakiwapa vijana wenye sifa za kulitumikia Taifa lao na kujenga maisha yao kupitia ajira hizo.

“Mheshimiwa Rais,mabadiliko haya makubwa yaliyofanyika ndani ya muda mfupi yataacha alama na kumbukumbu kubwa kwetu familia ya Jeshi la Polisi na kizazi kijacho cha watanzania na daima utakumbukwa kwa mambo haya uliyoyatenda kipindi hiki cha uongozi wako.

“Nakuomba Mheshimiwa Rais,pokea hadithi,hii ni hadithi nzuri,hii ni hadithi njema,tunaisimulia mbele yako na wewe ukiwepo na tutaendelea kukusimulia hadithi hizi nzuri kila tutakapokuwa pamoja na wewe ili watanzania wazisikie ,ili watanzania waone yale tunayoyaongea.

“Sasa hivi si muda wa kuuziana mbuzi kwenye gunia mambo yote yako hadharani”amesema IGP Wambura

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 16,610
  • Total page views 18,848

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In