• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Rais Mstaafu Kikwete akutana na msichana aliyefanyiwa upasuaji wa moyo akiwa na miaka minne,sasa ni Mwanafunzi Shahada ya Udaktari

by bajeti
May 29, 2026
in Habari
0
Rais Mstaafu Kikwete akutana na msichana aliyefanyiwa upasuaji wa moyo akiwa na miaka minne,sasa ni Mwanafunzi Shahada ya Udaktari
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

RAIS Mstaafu wa  awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amekutana na msichana Catherine  Minja aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio akiwa na umri wa miaka minne  katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa  Muhimbili  (MOI) miaka 18 iliyopita.

Rais Mstaafu Kikwete amekutana na Minja Mei 29,2026 jijini    Dar es Salaam ambaye sasa ameshakuwa msichana mkubwa ambapo alifanyiwa upasuaji wakati huo madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) walikuwa wakitumia majengo ya MOI kabla jengo lao halijakamilika.

Rais Mstaafu Kikwete na Catherine Minja walikutana kwa mara ya kwanza Mara ya Novemba 14, 2008 wakati Dkt. Kikwete akiwa Rais alipokwenda kumjulia hali Catherine  hapo MOI baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hiyo.

Wakati huo Catherine alikuwa mmoja wa wagonjwa wa mwanzo kufanyiwa upasuaji huo katika taasisi hiyo.

Miaka 18 baadaye, Minja  amekua na sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Kairuki  jijini Dar es Salaam.

Minja alifika ofisini kwa Rais Mstaafu Kikwete kumsalimia na kumshukuru kwa mchango wake katika kuanzisha na kuimarisha huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.

Dkt. Kikwete amempongeza Minja kwa kutimiza ndoto yake ya kusomea udaktari, jambo ambalo aliahidi kulifanya alipokuwa mtoto.

Amesema amefurahishwa kumuona akiwa mwenye afya njema na akijiandaa kulitumikia taifa kupitia taaluma ya tiba.

Kwa upande wake, Minja amesema anatamani kuwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ili kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto kama aliyowahi kupitia yeye mwenyewe, akieleza kuwa hiyo itakuwa ni moja ya njia ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha na afya njema

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:19
  • Today's page views 19
  • Total visitors 16,612
  • Total page views 18,850

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In