• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 24, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Ongezeko la joto laitesa Canada

by BAJETI
August 16, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

OTTAWA,CANADA

CANADA inapambana kuuzima moto unaondelea kuwaka katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ambao unaosababishwa na kuongezeka kwa viwango vya joto.

Katika Jimbo la British Columbia la nchi hiyo, serikali imetangaza kuwa kuna moto unaowaka katika maeneo 269 ambapo 61 tu ndio umedhibitiwa.

Moto huo unawaka zaidi katika maeneo ya kati na kusini mwa jimbo hilo karibu na mpaka na jimbo la Alberta.

Canada imekumbwa na joto kali linalofikia nyuzi joto 46.1 hali iliyosababisha migahawa, maduka  na shule kufungwa katika baadhi ya maeneo.

Mbali na kufungwa kwa shule na shughuli zingine za kijamii theluji pia imeyeyuka na kusababisha kuongezeka kwa kina cha maji ya mto, hali iliyopeleka wananchi kuhamishwa.

Wimbi hilo la joto, limeathiri zaidi magharibi mwa nchi hiyo, limesababisha msimu wa joto mkali zaidi katika miaka 84 iliyopita nchini humo.

Kulingana na Huduma ya Hali ya Hewa ya Canada, joto la nyuzi 46.1 lililorekodiwa katika jimbo la British Columbia.

Rekodi ya awali ya joto la juu katika historia ya nchi hiyo ilikuwa nyuzi 45 Celsius, iliyorekodiwa katika jimbo la Saskatchewan mnamo Julai 1937.

Awali mtaalam wa hali ya hewa katika Wizara ya Mazingira ya nchi  hiyo  Derek Lee,    ,alikielezea chombo cha habari cha  CBC kuwa joto litapanda zaidi kutoka nyuzi 46.1 hadi kuweza kufikia nyuzi joto  50 za Celsius katika maeneo mengine.

Next Post

Moto waibukia Ufaransa,maelfu ya watu wahamishwa

Ugiriki yaelemewa na moto wa msituni

DC Mjema awafunda TRA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,388
  • Total page views 18,592

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In