• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, April 30, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

SMT:Ukosefu wa nidhamu unasababisha miradi kutokalimika

by bajeti
July 11, 2022
in Mazingira
0
SMT:Ukosefu wa nidhamu unasababisha miradi kutokalimika

Mwenyekiti wa Shirika la Maeendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani Augustino Noto(mwenye suti nyeusi katikati) akiwa na viongozi na Wakuu wa Idara mbalimbali mara baada ya kikao kazi cha kujadili miradi ya mazingira iliyo chini ya shirika hilo wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani hivi karibuni(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO,PWANI

 

MWENYEKITI wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani, Augustino Noto amesema nidhamu ndio jambo muhimu katika kufikia malengo kwa kuwa sheria hazipo serikalini pekee bali hata kwa mashirika binafsi.

Hata hivyo Noto ameongeza kuwa miradi mingi inashindwa kufanikiwa kutokana na kukosekana kwa nidhamu za viongozi na wafanyakazi  kwa kuwa hawakosi visingizio pindi mambo yanapoharibika

Noto ametoa kauli hiyo juzi wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali wanaohudumu chini ya ofisi yake.

Amesema Ofisi hiyo ya Mkoa ina jumla ya wafanyakazi 25 wakiwemo wakuu wa idara za Habari,Mazingira,Mipango na Fedha  Elimu na zingine ambapo kazi kubwa walizonazo ni kuhakikisha mkoa huo kupitia SMT, unafanya vizuri katika suala la mazingira.

“Ni lazima tuwe na nidhamu katika kutekeleza majukumu yetu wote ili kufikia malengo tuliyojiwekea katika kufanikisha malengo ya miradi iliyopo ili kuleta tija kwa wananchi na serikali kwa ujumla,”amesema Noto

Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani Augustino Noto(katikati)akizungumza na wakuu wa idara ya ofisi yake (hawapo pichani) jana wakati wa kikao kazi juu ya kuendeleza miradi ya mazingira katika mkoa huo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa SMT Mkoa wa Pwani John Naggar na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa SMT Mputo Sufiani.Picha na Goodluck Hongo.

Noto amebainisha kuwa mazingira ndio kipaumbele cha SMT hivyo kila mwana SMT ni muhimu kuhakikisha kuwa mazingira yanalindwa katika eneo lake ili kuisaidia serikali na wananchi.

Kwa    upande wake, Katibu Mkuu wa SMT Mkoa wa Pwani John Naggar, amesema SMT Mkoa wa Pwani inahudumia halmashauri tisa ikiwemo  Mkuranga,Kisarawe,Rufiji,Kitibi,Kibaha Mjini,Bagamoyo,Chalinze  hivyo kila mkuu wa idara ngazi ya mkoa  na kazi kubwa ya kufanya ndani ya halmashauri hizo.

Naye Naibu Katibu wa SMT Mkoa wa Pwani Geofrey Katunzi, amewataka wakuu hao wa idara kukufanya vikao vya mara kwa mara na wenzao ngazi ya wilaya ili kufikia malengo na mikakati ya shirika hilo.

mwisho

Next Post
Wanahabari:Bodi ya Ithibati  ya Habari iundwe na wanataaluma husika.

Wanahabari:Bodi ya Ithibati ya Habari iundwe na wanataaluma husika.

Serikali kuwachukulia hatua waingizaji vifaranga kwa magendo

Serikali kuwachukulia hatua waingizaji vifaranga kwa magendo

Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:12
  • Today's page views 13
  • Total visitors 15,997
  • Total page views 18,152

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In