• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, January 9, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Rais Samia kufungua mkutano wa 65 wa UNWTO

by bajeti
October 5, 2022
in Mazingira
0
Rais Samia kufungua mkutano wa 65 wa  UNWTO

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mkutano wa 65 wa UNWTO unaoanza leo Oktoba 5,2022 jijini Arusha.Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika (65th UNWTO-CAF Meeting) unaoanza leo Oktoba 5, 2022 jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha.

Amesema lengo la mkutano huo ni kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la ugonjwa wa UVIKO-19 uliokuwa umeathiri utalii wa kimataifa kwa wastani wa kati ya asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Aidha, ameongeza kuwa mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za Serikali katika kuongeza idadi ya watalii na kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii ya kimkakati hususani Utalii wa Mikutano na Matukio.

Balozi,Dkt.Chana amefafanuwa kuwa mkutano huo utawezesha kujengea uwezo wataalam na wadau wa utalii katika kutangaza utalii, kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabaha ya kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano na mapato ya Dola za Marekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.

“Mkutano huo ni nyenzo mojawapo ya kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,katika kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kupitia programu ya Tanzania – The Royal Tour”amesema Balozi Dkt. Chana.

Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wa utalii wakifuatilia taarifa wakati wa mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha Oktoba 5,2022.(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

Mkutano huo wenye Kauli Mbiu ya “Kuujenga Upya Utalii Stahimilivu wa Afrika kwa Maendeleo Jumuishi ya Kiuchumi na Kijamii”. utahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirika hilo  Zurab Pololikashvili na kukutanisha mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka nchi wanachama wa UNWTO wa Kanda ya Afrika zaidi ya 50.

Mbali na hao lakini pia wadau wengine wakiwemo wataalam wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda, watoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa utalii, wawekezaji, pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.

Next Post
Rais Samia atoa bilioni mbili ujenzi vyumba vya madarasa Arusha

Rais Samia atoa bilioni mbili ujenzi vyumba vya madarasa Arusha

Serikali yaanzisha miradi 76 ya Utalii na Utamaduni

Serikali yaanzisha miradi 76 ya Utalii na Utamaduni

Mhagama:Serikali kusimamia mikakati kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja

Mhagama:Serikali kusimamia mikakati kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 23
  • Total visitors 13,006
  • Total page views 14,750

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In