NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amesema miradi 76 ya Utalii wa Utamaduni imeanzishwa katika Kanda za Kaskazini, Kusini na Kanda ya Ziwa ambazo zinaendelea kutangaza nchi ya Tanzania.
Balozi Dkt.Chana amesema hayo Oktoba 07, 2022 jijini Arusha wakati akitoa salamu za wizara yake katika Uzinduzi wa Tamasha la Maasai Festival litakalofanyika mwaka 2023, ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul.
“Wizara imetenga eneo la Makumbusho lililopo Dar es Salaam kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Utamaduni ikiwemo Mila, Desturi, vyakula, na mavazi” amesema Balozi Dkt.Chana.
Balozi Dkt.Chana ameongeza kuwa, Maasai Festival ni moja ya mazao ya Utalii wa Utamaduni ambayo yatasaidia kutangaza nchi vyema na kuongeza idadi ya watalii kutembelea vivutio vya nchi na kuongeza pato la Taifa.
Tamasha hilo ni miongoni mwa matamasha ambayo yanafanyika nchini kwa lengo wa kuhamasisha, kutangaza na kurithisha Utamaduni wa Watanzania.




Discussion about this post