NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof.Anna Tibaijuka amewataka wazazi nchini kuwa makini na mitandao ya kijamii katika malezi ya watoto wao.
Amesema katika wakati huu wa utandawazi na kukuwa kwa technoljia duniani inayoifanya kuwa kijiji kimoja kuna mianya mingi ya kuporomosha maadili ya mila na desturi na hasa vijana wa kati ya umri wa miaka 15 hadi 25.
Prof.Tibaijuka ametoa onyo hilo Oktoba 15,2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Mother of Mercy katika mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo.
Amesema kundi hilo la watoto ndio linaloathirika zaidi na mitandao ya kijamii hivyo ni muhimu kwa wazazi kukaa mbali na watoto pindi wanapotumia akaunti za mitandao yao.
“Ni lazima kuwa makini na hili na usiwaachie wajifunze vitu ambavyo wewe hujui, ni vema ukavijua na ukaweza kumpa mwanao tahadhari kwa jambo husika”amesema Tibaijuka
Tibaijuka ameongeza kuwa licha ya umuhimu wa mitandao kuwa na fuksa za ajira,elimu na biashara ya kwa watu wenye umri mkubwa zaidi lakini kwa watoto ni muhimu ikajulikana anatumia kwa malengo ya kuelimika na si vinginevyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule hiyo Regina Rwegasira amesema licha ya kufundisha lakini pia kipaumbele chao kingine ni nidhamu kuanzia wanafunzi,walimu hadi wafanyakazi wa shule.
“Shule haiwezi kumvumilia mwalimu au mtumishi anayekiuka maadili lakini pia tunafundisha watoto kumjua mungu kwa kila mwanafunzi na imani yake ya dini ili kuwa watoto bora wanapokwenda katika jamii”amesema Rwegasira
Hata hivyo Rwegasira amefafanuwa kuwa licha ya mtoto kumaliza katika shule yao lakini wana mfumo wa kuwafuatili huko wanakokwenda ili kuwasaidia zaidi kitaaluma ili kuwa na kizazi bora kwa Taifa.
Shule ya Mother of Mercy imejipatia umaarufu kwa kutoshuka nafasi ya 10 bora katika maotokeo ya Mkoa Dar es Salaam na kushika nafsi za juu kwa mitihani ya kitaifa.





Discussion about this post