NA MIRIAM SARAKIKYA, ARUSHA.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kusimamia Sera,Mipango na mikakati ili kusaidia kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja .
Ameyasema hayo Oktoba 10,2022 mkoani Arusha wakati akizindua Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mhagama amesema katika kusimamia sera , mipango na mikakati yote ya serikali wanaamini kuwa itaongeza faida fungamanishi kwa wananchi na kuleta uchumi wa pamoja na wa jumla.
Ameongeza kuwa kutasaidia kufungua uchumi wa wananchi ili nchi iweze kuwa na kipato cha juu na kuondoka kwenye uchumi wa kati.
Mahagama amewataka watumishi wote wa kituo hicho kuonyesha mfano na umuhimu wake kwa kutoa huduma bora na kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha.
Awali akitoa taarifa ya kituo hicho Mratibu wa Urasimishaji wa Biashara nchini Dr Seraphia Mgembe amesema wameweza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara ya namna ya kufanya biashara ambapo lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya biashara zinazokua.
Naye Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Arusha Eni Mwanga ameeleza kuwa kituo hicho kitasaidia wananchi kupata elimu ya mlipa kodi pamoja namba ya utambulisho (TN) ili wafanyabiashara hao waweze kufanya kazi zao kwa amani na utulivu.




Discussion about this post