• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, May 2, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Masanja:Onesho la SITE kufungua fursa ya Utalii Dar es Salaam

by bajeti
October 23, 2022
in Habari
0
Masanja:Onesho la SITE kufungua fursa ya Utalii Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (kushoto) akiwasili katika Maonesho ya sita ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili (SITE) yanayomalizika leo Oktoba 23,2022 jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Maliasili na Utali)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja amesema uwepo Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili (SITE) katika Jiji la Dar es Salaam ni fursa kubwa kwa jijini hilo kutangaza vivutio vyake.

Amesema Jiji la Dar es Salaam ndio lango Kuu la Biashara Tanzania na kwamba wageni wengi wanaofika nchini wanafikia katika Jiji hilo na kisha kuelekea kwenye maeneo mengine ya Utalii.

Masanja ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Oktoba 21,2022 wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kunakofanyika Onesho la S!TE 2022.

Aidha ameeleza kuwa Jiji la Dar es Salaam lina historia ya kipekee kutokana na vivutio vilivyopo vya kiutamaduni ikiwemo majengo na malikale.

“Jiji la Dar es Salaam lina historia kubwa na nzuri ya kiutalii kutokana na uasilia wake,kuna maeneo mengi ya kiutalii ikiwemo majengo na malikale hivyo Onesho hili litafungua fursa za kiutalii katika Jiji hili” amesema Masanja.

Akizungumzia Onesho hilo linalotarajia kumalizika rasmi leo Oktoba 23, 2022, Naibu Waziri huyo amesema lengo kuu la onesho hilo ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania, na kukutanisha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za utalii wa Kitaifa na Kimataifa.

Next Post
Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 8
  • Total visitors 16,033
  • Total page views 18,191

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In