• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, May 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

by bajeti
May 25, 2023
in Habari
0
Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

SERIKALI  imesema inaendelea na jitihada za kuzitafutia ufumbuzi hoja nne za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizobaki  ili kuhakikisha kuwa unaendelea kudumu na kuimarika,

Hayo yameelezwa Mei 24,2023 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu  Latifa Khamis Juwakali.

Pinda amezitaja hoja hizo zilizobaki kuwa ni pamoja na Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Usajili wa Vyombo vya Moto na Uingizaji wa sukari inayozalishwa Zanzibar katika Soko la Tanzania Bara.

Hoja nyingine ni Mgawanyo wa mapato yatokanayo na hisa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na faida ya Benki Kuu.

“Hoja hizo nne zilizosalia zipo katika hatua mbalimbali za majadiliano na ni matumaini ya Serikali zetu mbili kuwa changamoto zote zitapatiwa ufumbuzi na hivyo sote tutafaida matunda ya Muungano,” amesema Pinda.

Ameongeza kuwa kwa msingi huo wizara zinazohusiana na masuala ya Muungano hukutana kwa ajili ya kujadili changamoto zinazokabili sekta zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Desemba 6,2022 jumla ya hoja nne zilipatiwa ufumbuzi katika kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kilichofanyika jijini Dodoma.

Hoja zilizopatiwa ufumbuzi katika kikao hicho ni pamoja na Malalamiko ya Wafanyabiashara wa Tanzania Zanzibar kutozwa kodi mara mbili wanapoagiza mizigo kutoka nje ya nchi na kupeleka Tanzania Bara, Kodi ya Mapato na Kodi ya Zuio,Ongezeko la Gharama za Umeme kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwenda Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) pamoja na Hoja ya Mkataba wa Mkopo wa Fedha za Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (Terminal III).

 

Next Post
Wachina kulipa nauli kupitia kiganja cha mkono

Wachina kulipa nauli kupitia kiganja cha mkono

MISRI

MISRI

Serikali yaanzisha kampeni ya “SOMA NA MTI”

Serikali yaanzisha kampeni ya "SOMA NA MTI"

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 13
  • Total visitors 16,190
  • Total page views 18,361

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In