• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali yaanzisha kampeni ya “SOMA NA MTI”

by bajeti
May 27, 2023
in Mazingira
0
Serikali yaanzisha kampeni ya “SOMA NA MTI”

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis (katikati) akipanda mti wakati wa halfa ya zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Sekondari Buigiri iliyopo Kata ya Buigiri Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoani Dodoma Mei 26, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

SERIKALI kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeanza kampeni ya kupanda miti mashuleni ijulikanayo kama “SOMA NA MTI”  ili kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Aidha upandaji miti na uhifadhi wa misitu ni moja ya hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi, hivyo kwa kutambua umuhimu huo Serikali imeamua kuanzisha “SOMA NA MTI“

Hayo yameelezwa Mei 26, 2023 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Khamis Hamza Khamis wakati wa hafla ya zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Buigiri iliyopo Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma, na kuongeza kuwa suala la uhifadhi wa mazingira ni jambo mtambuka linalohitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwafanya wanafunzi waone zoezi la upandaji miti kuwa ni sehemu ya maisha yao ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame na uhaba wa maji.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi nchini katika kuhakikisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira inakuwa na mafanikio ikiwemo kuwawezesha vijana kupata elimu sahihi ya utunzaji wa miti na kuchangia uhifadhi wa mazingira kwa weledi.

“Mabadiliko ya tabianchi ni ongezeko la muda mrefu la joto la wastani la dunia na kusababisha kubadilika kwa mfumo mzima wa hali ya hewa, ili kuinusuru jamii yetu kutoka kwenye changamoto hizi tunapaswa kupanda miti kwa wingi ili kuokoa maisha ya viumbe hai wengine pamoja na binadamu” amesema Khamis.

 Hata hivyo Khamis amevitaka vyombo vya habari, taasisi na wadau wa mazingira  kuendelea kutoa elimu kwa  wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amebainisha kuwa viongozi wakuu wa dunia kila wakutanapo katika vikao na mikutano mbalimbali hujadili kwa kina masuala muhimu ya kidunia ikiwemo ajenda ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ambapo umuhimu wake unabeba mustakabali wa viumbe hai, rasilimali na maliasili zilizopo katika uso wa dunia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirika la Tabora Carbon Credit Harvest (TCCHP) Bernard Mwanawille amesema Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira ikiwemo uhamasishaji wa jamii katika zoezi upandaji wa miti.

“Pamoja na kuhamasisha jamii uhifadhi na utunzaji wa mazingira, mwaka 2019 Shirika letu limeingia mkataba na Serikali katika uzalishaji wa biashara ya kaboni katika Mkoa wa Tabora ambayo tayari tumepatiwa misitu ya serikali ya mkoa na Wilaya” amesema Mwanawille.

Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Riziki Lulida amesema ajenda ya Dodoma ya kijani na Tanzania ya kijani inawezekana iwapo kutakuwepo ushirikiano wa pamoja baina ya serikali, jamii na wadau katika suala la uhamasishaji wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Next Post
Ndege kubwa ya abiria iliyotengenezwa na China yasafiri kwa mara ya kwanza

Ndege kubwa ya abiria iliyotengenezwa na China yasafiri kwa mara ya kwanza

Biashara haramu ya wanyama na mimea pori yashika nafasi ya nne duniani

Biashara haramu ya wanyama na mimea pori yashika nafasi ya nne duniani

Serikali kuwapa mikopo vijana waliojifunza uvuvi na ukuzaji viumbe maji

Serikali kuwapa mikopo vijana waliojifunza uvuvi na ukuzaji viumbe maji

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In