HELSINK,FINLAND
FINLAND inatarajia kuzinyima misaada baadhi ya nchi za kiafrika kutokana na kutoonesha kuipinga Urusi baada ya kuanzisha kile inachokiita oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine.
Nchi za Kiafrika ambazo zinaiunga mkono Urusi katika mzozo wa Ukraine zitapoteza msaada wa maendeleo kutoka Finland.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Juni 21,2023 na Tovuti ya habari ya RT,Serikali ya Finland inataka kupunguza misaada ya maendeleo kwa karibu dola bilioni moja na kwamba Mataifa yanayoendelea yanapaswa kuzingatia maendeleo yao ya ndani badala ya kuunga mkono vita vya Urusi.
Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Taifa la nchi hiyo(YLE) Juni 19,2023,Waziri wa Biashara ya Nje na Maendeleo wa nchi hiyo, Ville Tavio amesema ni wajibu wa msingi wa nchi yake ni kuunga mkono Ukraine na ni makosa kimaadili kwa nchi zinazounga mkono “uchokozi” wa Urusi dhidi ya Kiev kuendelea kupokea misaada ya maendeleo kutoka Finland.
“Ninaangalia nchi zinazopokea misaada kutoka Finland, lakini nichague kutoheshimu utaratibu unaozingatia sheria za kimataifa na Mamlaka ya Serikali ya Ukraine,” amesema Tavio.
Hata hivyo Tavio hakutaja nchi zitakazonyimwa misaada hiyo ya maendeleo ambapo baadhi nchi kama Ethiopia, Kenya,Somalia, na Msumbiji ni washirika wakuu wa Finland barani Afrika, ambazo hukupokea misaada kutoka nchi hiyo kwa muda mrefu.
Nchi kadhaa za Kiafrika,ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, zimesalia kutofungamana na mzozo kati ya Urusi na Ukraine, licha ya shinikizo la nchi za magharibi kuzitaka kuunga mkono Ukraine.




Discussion about this post