• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Wabunifu waishukuru Serikali kuwapatia Sh.Bilioni 1.191

by bajeti
June 25, 2023
in Sayansi na Teknolojia
0
Wabunifu waishukuru Serikali kuwapatia Sh.Bilioni 1.191

Mbunifu na Mtafiti wa Kaboni inayotokana na vifuu vya nazi Tiberius Mario(wa tatu kulia)akipokea hundi ya fedha kwa niaba ya wabunifu wenzake 48 kutoka kwa mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka wakati wa Kongamano la nane la Sayansi, Teknolokojia na Ubunifu(STICE) Juni 16,2023 jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Amos Nungu(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

BAADHI ya watafiti na wabunifu wa vitu mbalimbali vya sayansi na kiteknolojia wameishukuru Serikali kwa kuwapatia kiasi cha Sh. Bilioni 1.191 zitakazosaidia kuendeleza bunifu zao.

Mbali na kiasi hicho lakini pia Serikali imetoa kiasi cha Sh.Bilioni 2.5, kwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili zitumike kuwakopesha wabunifu.

Kutolewa kwa fedha hizo na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan zitasaidia katika kuongeza soko la ajira ambapo wabunifu hao watazitumia kuajiri vijana wenzao katika kuendeleza bunifu zao.

Akizungumza na Bajeti Communication jijini Dar es Salaam Juni 24,2023,Mbunifu na Mtafiti wa Kaboni inayotokana na vifuu vya nazi Tiberius Mario amesema anaishukuru sana Serikali kutoa kiasi hicho cha fedha ambapo kitagawanywa kwa wabunifu 49.

Amesema yeye alipokea hundi ya kiasi cha Sh.Bilioni 1.10 kwa niaba ya wenzake 48 wakati wa Mkutano wa Kimataifa na Maonesho ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yaliyofanyika Juni 14 hadi 16 jijini Dar es Salaam.

Mario ambaye alikuwa mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Kitaifa ya Ubunifu,Sayansi na Teknolojia (MAKISATU) kwa mwaka 2022 jijini Dodoma na kupata fursa ya kupewa zawadi na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema yeye binafsi na wenzake wamepata faraja kuona serikali inawathamini.

“Fedha hizo ingawa bado hatujakabidhiwa lakini si kazi rahisi kwa kuwa licha ya kuwa wabunifu lakini tulionesha tena ubunifu wetu katika maonesho hayo ambapo tulikuwa 20 na tuliobahatika kuchaguliwa ni saba hivyo tukajumuishwa na wenzetu wengine na tukafikia 49.

“Si unapewa fedha tu bali unachofanya lazima kionekane hivyo hata tukichukua fedha hizo lazima kuwe na nidhamu japokuwa si mkopo ili utakapoomba tena uweze kupewa.”amesema Mario

Awali akizungumza Machi 8,2023 mbele ya waandishi wa habari na watafiti jijini Dar es Salaam wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa habari na watafiti yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH),Mario amesema Tanzania inauwezo wa kuokoa dola za kimarekani Milioni sita za kuagiza Kaboni kutoka nje ya nchi.

Amesema Tanzania ni nchi ya 16 duniani kwa kuzalisha nazi baada ya nchi kama Indonesia,India,Brazil na Ufilipino hivyo kuna kiwango kikubwa cha nazi na ni fursa pia kwa watanzania kujua kuwa vifuu vya nazi ni mali inayoweza kuzalisha Kaboni.

“Baada ya kumaliza Chuo nilianza kufanya utafiti wa kuzalisha Kaboni na ndipo nilipobuni uzalishaji kwa kutumia vifuu vya nazi na baada ya kupimwa na kuthibitishwa imeonekana kuwa na uwezo wa asilimia 98 kukamata madini yaliyopo katika udongo”amesema Mario

Amesema kila mgodi wa dhababu lazima uwe na Kaboni kwa ajili ya kusaidia kukamatisha dhababu na Tanzania inahitaji tani 1500 pekee za Kaboni ambazo asilimia kubwa huingizwa kutoka nje ya nchi.

 

Next Post
“Nyumbu na Tembo vinara kutumia shoroba”

"Nyumbu na Tembo vinara kutumia shoroba"

Urusi yaichanganya dunia,EU yasema sasa ni hatari zaidi kuliko awali

Urusi yaichanganya dunia,EU yasema sasa ni hatari zaidi kuliko awali

DODOMA

DODOMA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In