MOSCOW,RUSSIA
MACHO ya dunia yameelekezwa nchini Urusi baada ya Kiongozi wa Kampuni binafsi ya Kijeshi Wagner Group Evgeny Prigozhin kuasi na kuapa kupambana na majeshi ya Urusi wakati nchi hiyo ikiwa katika oparesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine iliyoianzisha Februari 24,2022.
Hata hivyo Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema jaribio la mapinduzi lililofanywa na Prigozhin ni uhaini na kwamba wanauzoefu wa hali kama hizo na watailinda nchi yao dhidi ya uhaini.
Wakati Rais Putin kauli hiyo ,usalama unaidaiwa kuimarishwa jijini Moscow na maeneo mengine ya Urusi huku vikosi vya jeshi la nchi hiyo vikishambulia magari ya msafara wa Kiongozi wa Kampuni Binafsi ya Kijeshi ya Wagner Group Evgeny Prigozhin
Rais Putin ametoa hotuba hiyo kwa taifa Juni 24,2023 jijini Moscow muda mfupi baada ya vikosi vya Prigozhin kuvuka mpaka kutoka Ukraine walikokuwa wakipigana na kisha kuliteka jiji la Rostov-on-Don kusini mwa Urusi.
Amesema jaribio la uasi lililofanywa na mkuu wa kampuni ya kijeshi ya kibinafsi ya Wagner, Evgeny Prigozhin, ni sawa na usaliti kwa Urusi na watu wake na kuapa kwamba vyombo vya kutekeleza sheria nchini vitachukua hatua madhubuti kurejesha utulivu.
Alibainisha kuwa Moscow inahusika katika mapambano ya kihistoria ya kulinda mustakabali wake huku “ikizuia uchokozi kutoka kwa Wanazi mamboleo na mahasimu wao kutoka katika nchi za Magharibi.
“Tunapigania maisha na usalama wa watu wetu, uhuru na uhuru wetu,kwa haki ya kuwa na kubaki Urusi na kwamba vikosi vya Wanajeshi vya Urusi na mashirika mengine ya serikali yamepokea maagizo muhimu na hatua madhubuti zitachukuliwa ili kuleta utulivu katika Rostov-on-Don,” kusini mwa Urusi”amesema Rais Putin

Wakati huo Idara ya Usalama wa Taifa (FSB)imefungua kesi ya jinai dhidi ya Prigozhin, kwa madai ya kutetea uasi dhidi ya serikali.
Awali, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilishumtumu Prigozhin kwa kueneza uwongo juu ya video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii iliyodai kuwa jeshi la Urusi lilishambulia kambi ya wapiganaji wa Wagner.
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu ilisema kwamba uhalifu huo unaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha miaka 12 hadi 20.”
Hata hivyo ikiwa vikosi vya Urusi vitafanikiwa kuzima jaribio hilo na kuchukua uthibiti wa jiji la Rostov-on-Don kusini mwa nchi itadhihirisha uwezo wake wa kijeshi.




Discussion about this post