• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 4, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Russia yatishia kuligeuza Jiji la Kiev,Ukraine kuwa’’ lundo lililoyeyushwa’’

Yaonya Marekani haitasalimika ikiwa vita vya nyuklia vitazuka barani Ulaya

by bajeti
September 15, 2024
in Habari
0
Russia yatishia kuligeuza Jiji la Kiev,Ukraine kuwa’’ lundo lililoyeyushwa’’

Silaha za nyuklia za Russia

Share on FacebookShare on Twitter

MOSCOW,RUSSIA

RAIS wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev, ametishia kutumia silaha zisizo za nyuklia zenye uwezo wa kuugeuza Mji Mkuu wa Ukraine, Kiev, kuwa “rundo lililoyeyushwa” wakati ustahimilivu wa Moscow utakapomalizika.

Medvedev ambaye ni Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia amesema kuwa nchi yake inaweza kuuangamiza kabisa mji mkuu wa Ukraine, Kiev, kwa silaha mpya zenye teknolojia ya hali ya juu katika kukabiliana na matumizi ya Ukraine ya makombora ya masafa marefu ya nchi za Magharibi.

Rais huyo wa zamani wa Russia ameeleza kuwa, nchi yake tayari ina sababu rasmi za kutumia silaha za nyuklia, lakini hadi sasa imechagua kutofanya hivyo.

Medvedev amekuwa akizitutumu nchi za Magharibi kuwa zinachochea vita vya nyuklia vyenye uharibifu mkubwa kwa sababu ya kuendelea kuiunga mkono kijeshi Ukraine katika vita vyake dhidi ya Russia.

Kwa upande wake balozi wa Russia mjini Washington, Anatoly Antonov, amesema kuwa Marekani haitasalimika na mzozo wowote wa nyuklia unaoweza kuzuka barani Ulaya.

Antonov ametoa wito kwa utawala wa Marekani kuacha kucheza na maneno

Hata hivyo uwezekano wa matumizi ya silaha za maangamizi za nyuklia ni mkubwa kutokana na mfumo wa nchi za Magharibi unaoongozwa na Marekani kutengeneza miungano ya kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na nchi zinazoonekana kwenda kinyume na maslahi ya nchi hizo

NATO dhdi ya RUSSIA

Marekani na washirika wake wa nchi za ,Magharibi walianzisha Jeshi la NATO ili liweze kukabiliana na Russia  ambapo zaidi ya nchi 30 zimejiunga katika umoja huo wa kijeshi zikiwemo nchi zilizokuwa katika Umoja wa Kisoviet (USSR)

Washirika wa NATO wakiongozwa na Marekani ndio watoaji wakubwa wa silaha kwa Ukraine ambapo lengo lao ni kuhakikisha kuwa Russia inashindwa vita vyake ilivyoviazisha shidi ya Ukraine

Marekani,Korea Kusini  na Japan dhdi ya Korea Kaskazini

Nchi hizo zikiongozwa na Marekani zimeunda muungano huo wa kijeshi ili kukabiliana na Korea Kaskazini ambayo imekuwa ikijihami kwa kutengeneza makombora ya nyuklia na kufanya majaribio mara kwa mara.

Marekani,Taiwani,Ufilipino dhidi ya China

Marekani na Ufilipino zimekuwa zikifanya mazoezi makubwa ya kijeshi mara kwa mara katika kile kinachoelezwa kukabiliana na ushawishi wa China katika bahari ya China Kusini.

Hata hivyo Marekani imekuwa ikiiuzia silaha Taiwan ambayo China inaeleza kuwa ni sehemu yake na ipo siku itakichukua kwa nguvu kisiwa hicho kinachojitawala chenyewe jambo linalofanya eneo hilo nalo kuwa katika fukuto la vita

Marekani,Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Iran

Marekani na washirika wake wamekuwa wakianzisha kambi za kijeshi katika nchi za kiarabu ili kukabiliana na ushawishi wa Iran katika eneo hilo la Mashariki ya Kati

Marekani na washirika wake wamekuwa wakipeleka silaha nzito ikiwemo meli ya kubebea ndege katika eneo la Pasific kukabiliana na kile kinachoelewa kuwa kitisho cha Iran dhidi ya Israel

Hata hivyo Iran imekuwa ikilalamika kuhusu kuhujumiwa kwa miradi yake ya kutengeneza Nyuklia kwa ajili ya matumizi ya amani lakini Marekani na washirika wake wa nchi za Magharibi hawataki ili hali Israel na baadhi ya nchi za kiarabu zinamiliki silaha hizo.

Hata hivyo mbali na miungano hiyo ya kijeshi inayoongozwa na Marekani katika kila pembe ya dunia,imekuwa ikiweka vikwazo vingi dhidi ya mataifa ambayo hayafungamani na utamaduni wa Marekani na nchi za Magharibi

Kutoka vitendo hivyo vya nchi za Magharibi na Marekani za kuunda miungano ya kijeshi na kuweka vikwazo kwa nchi zisizofuata demokrasia na matakwa yao imesababisha kutokea kwa vita katika baadhi ya maeneo duniani ikiwemo Urusi na Ukraine na Kundi la Hamas linalotawala Ukanda wa Ghaza na Israel

Mbali na vita hivyo lakini pia Urusi,Korea Kaskazini,Iran na China zimeamua kuungana kijeshi na ikiwa Marekani na Mataifa ya Magharibi watajaribu kuzishambulia nchi hizo kutokana na miungano yao ya kieshi basi kauli ya Urusi ya kugeuzi mji mkuu wa Ukraine,Kiev, kuwa lundo lililoyeyushwa zitakuwa za kweli na sio hadithi.

Mbali na hilo lakini pia Mataifa hayo yanayoonekana kuwa adui wa Nchi za Magharibi wataweza kuishambulia Marekani moja kwa moja kwa silaha za maangamizi ili kuifanya nchi hiyo kuonja athari za vita.

Marekani kwa miaka mingi haijawahi kupigana vita katika ardhi yake hivyo hutumia ardhi za nchi nyingine kushambulia maadui zao lakini ikiwa vita vitazuka basi Marekani inaweza kuingia katika historia ya kushambuliwa kwa nyuklia  kwa kuwa Urusi inaonekana iko tayari kufanya hivyo na haiogopi.

 

Next Post
TFC yakabidhi tani 61,000 za mbolea ya rukuzu

TFC yakabidhi tani 61,000 za mbolea ya rukuzu

DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

'Mapapa' wa biashara dawa za kulevya wahamia kwenye vyakula vinavyopendwa na watoto

TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,049
  • Total page views 18,208

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In