• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, May 26, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TARI,ZARI na NIBIO wajadili Afya ya Udongo

by bajeti
November 3, 2024
in Mazingira
0
TARI,ZARI na NIBIO wajadili  Afya ya Udongo

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imewakutanisha wadau mbalimbali wanaojishughulisha katika mnyororo wa thamani wa afya ya udongo  ili kubaini changamoto  zinazowakabili Wakulima pamoja na kuweka njia sahihi na endelevu za kutatua changamoto hizo kupitia mafunzo.

Hatua hiyo ni Utekelezaji wa Mradi unaolenga kujenga uwezo wa kitaasisi kwa Watafiti na maafisa ugani, pamoja na mafunzo kwa Wakulima juu ya afya endelevu ya udongo katika wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi.

Mradi huo wa miaka minne (2024-2027) unatekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) na Taasisi ya Norwegian Institute for Bio economy Research (NIBIO), kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Norway (Norad).

Akizungumza katika  ufunguzi wa Mkutano wa wadau, uliofanyika Oktoba 31, Jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana amesema Maabara hai ya afya ya  Udongo inalenga kutatua changamoto mbalimbali za afya ya udongo lengo ikiwa ni kumsaidia Mkulima kupata tija bila kuingia gharama zisizo lazima.

“Tukiwa na uhakika wa afya ya udongo maana yake tunaenda kumsaidia Mkulima kutambua namna sahihi ya matumizi ya viuatilifu, mbolea na Pembejeo zingine hata aina ya zao linalofaa eneo husika”  Amesema Dkt. Bwana.

Akieleza kuhusu mradi huo,Mratibu wa Mradi huo Dkt. Atugonza Bilaro, amesema Wilaya tatu  za Tanzania Bara ambazo ni  Kongwa kwa Mkoa wa Dodoma, Babati kwa Mkoa wa Manyara na Mbozi mkoani Songwe ambapo kwa  Zanzibar ni katika visiwa vya Pemba na Unguja ndio maeneo ambayo mradi huo utafanyika.

Dkt.Bilaro ambaye ni Mtafiti kutoka TARI amebainisha kuwa mradi huo unakuja na njia husishi ya Maabara Hai ya Afya ya Udongo ambayo inajumuisha Wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi tofauti za umma na binafsi wenye lengo moja la kutatua changamoto za afya ya udongo ili kumuongezea mkulima tija.

Naye Mkurugenzi wa NIBIO, Profesa Udaya Sekhar, amesema suala la  afya ya udongo ni muhimu katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Profesa Sekhar amesema kama suala la afya ya udongo halitaangaliwa kwa uzito unaostahili matokeo yake,tija kwa Mkulima itapungua na hata kuhatarisha suala la usalama wa chakula.

TARI na NIBIO wamekuwa na ushirikiano katika suala la Utafiti wa Kilimo ambapo mradi mwingine unaotekelezwa na Taasisi hizo mbili ni Mradi wa Kilimo Shadidi cha Mpunga.

Next Post
Serikali yapeleka mamilioni ya fedha kuimarisha kitengo cha maabara na mifupa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara

Serikali yapeleka mamilioni ya fedha kuimarisha kitengo cha maabara na mifupa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara

VETA yaanzisha kozi kwa wafanyakazi wa majumbani (house girl/boy)

VETA yaanzisha kozi kwa wafanyakazi wa majumbani (house girl/boy)

VETA yawakaribisha wastaafu kujifunza masomo ya ufundi stadi

VETA yawakaribisha wastaafu kujifunza masomo ya ufundi stadi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 16,499
  • Total page views 18,718

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In