• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

VETA yawakaribisha wastaafu kujifunza masomo ya ufundi stadi

Wajipanga kuwashawishi watoto wa kike kupenda ufundi

by bajeti
November 8, 2024
in Habari
0
VETA yawakaribisha wastaafu kujifunza masomo ya ufundi stadi

Lori la Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Mtwara linalotumika kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wao.(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO,MTWARA

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewakaribisha watu waliostaafu katika utumishi wao wa kazi kujiunga na mafunzo ya ufundi ili kuweza kuwapatia ujuzi pamoja na ujasiria mali wa kuweza kujiendeshe Maisha ya kustaafu

Kauli ya VETA imekuja wakati ambapo baadhi ya wastaafu wameanza kujiunga na baadhi ya kozi zinazotolewa na chuo hicho huku wengine wakihamasika kutaka kujiunga ili  kupata mafunzo ya ufundi stadi.

Kwa kudhihirisha hayo Bajeti Communication imefanya mazungumzo na mwanafunzi  ambaye ni mstaafu  anayesomea mafunzo ya mapishi mwaka wa pili Ester Mtumo ambaye ameeleza kujisikia furaha na amani kwani yeye amekuwa na ujuzi ambao utamsaidia kwenda kusimamia kazi zake pamoja kujipatia kipato.

Mtumo amebainisha kuwa aliamua kusomea fani hiyo baada ya kustaafu akiwa mtumishi wa umma na kisha kukaa nyumbani bila kazi.

‘’Kwa wastafu wenzangu mafunzo ya ufundi hayabagui umri pamoja na umri wangu VETA wameweza  kunifundisha ujuzi na nitaenda kuwa balozi mzuri kwa kufungua mradi wangu  na kusimania.

‘’Hivyo ni muhimu kwa wastafu kufika VETA  na kuchagua ujuzi ambao unaweza kumsaidia kuendesha maisha ya kila siku na kuondoka na adha zisizo za lazima”amesema Mtumo

Mwanafunzi ambaye ni mstaafu katika utumishi wa umma anayesomea mafunzo ya mapishi mwaka wa pili Chuo cha VETA mkoanji Mtwara Ester Mtumo akizungumza na mwandishi wa habari umuhimu kwa waastaafu kujiunga na VETA.

Amesema VETA ina fursa nyingi inazozitoa kupitia kozi zake zikiwemo za kupaka rangi,useremala na nyingine ambapo mtoto anaweza kusoma hadi chuo kikuu lakini akakosa mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanaweza kumsaidia sana.

‘’Wengi wananiuliza kwa umri wangu huu kwanini nasomea mapishi lakini katika kozi yangu hii niliyoanza 2023 na nitahitimu mwezi Desemba nimejifunza mambo mengi sana na nimegundua makosa mengi sana.

‘’Elimu haina mwisho na mtu anaweza kusoma hata akiwa mzee na akafanya vizuri na mimi nafanya hivyo kivitendo na natarajia baada ya kumaliza kozi yangu hii nitafungua bekari yangu ambapo naweza kuoka mikate na vitu vingine vingi’’amesema Ntumo

Ntumo ameongeza kuwa VETA kuna fani nyingi za watu wanaokaa nyumbani hivyo ni muhimu wakafika kupata ujuzi  kwani hata baadhi ya walimu waliostaafu kwa sasa nao wanataka kujiunga na chuo baada yeye kuchua hatua hiyo

Mfumo huo wa kuwafundisha ujasilimali watu waliostaafu utumishi wao unaweza kuliokoa  kundi hilo ambao wengi wao wanategemea kuishi kwa kiinua mgongo(Pension) hali inayowapeleka kuishi maisha magumu na ya kuhangaika.

Akizungumza na Bajeti Communication Oktoba 28,2024 mkoani Mtwara,Mkuu wa Chuo cha VETA mkoani humo Theresia Ibrahim amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa kila wilaya kunakuwa na Chuo cha VETA ili kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwani hakuna maendeleo bila mafundi.

Mkuu wa Chuo cha VETA mkoani Theresia Ibrahim

Amesema chuo kinaandaa mafundi ambao ni mahiri wanaoweza kujiari na kuajiriwa pamoja na kuwajiri wengine ,ikiwemo kushiriki kwenye kazi za maendeleo katika wilaya wana zotoka mfano ujenzi wa hospitali, shule na miradi mingine.

Ibrahim amefafanuwa kuwa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi hailengi watu,kundi wala kada fulani bali ni mafunzo ya watu wote ili mradi ahitaji mafunzo

”Mtanzania aliyestaafu tuna mpatia frusa   hapa kwetu VETA-Mtwara ya  kumfundisha ujuzi mdogo mdogo ambao anaweza kujishulisha akiwa nyumbani kwake  pamoja na mafunzo mjasiriamali ili kuwasaidia wastaafu hawa kusimamia pesa waliopata  kama pension kuendesha na kusimamia miradi midogo midogo kijasiriamali na endapo mstaafu atajishughulisha  ni moja ya mazoezi na kujipatia kipato pia.

 ‘’Tuna kozi za muda mrefu na mfupi zikiwemo za udereva wa malori na mabasi ya abiria na ya watu binafsi,kozi za viyoyozi na majokofu,tunafundisha uzalendo hasa kwa bodaboda,na sisi hapa tuna hoteli yetu ya VETA hivyo nayo inatumika kuwafundisha wanafunzi wetu

‘’Tunaanzisha mfumo wa kukaa na watoto wa kike hadi wafikie malengo yao,tunaruhusu pia mafundi wenye ujuzi wao kurasimisha ujuzi wao,tunafundisha pia ujasiriamali  lakini pamoja na kutoa mafunzo,tunatoa pia na huduma ya malazi kupitia hoteli yetu ya VETA-Mtwara’’amesema Ibrahim

Naye Mwalimu anayefundisha Kozi ya Food Producation Felister Shirima amesema wanafundisha pia kutengeneza vyakula vya asili vya kitanzania na vyakula kutoka mabara yote duniani

Mwalimu anayefundisha Kozi ya Food Producation wa Chuo cha VETA mkoani Mtwara Felister Shirima akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wao vyakula vya asili ya kitanzania na vya mataifa mengine duniani

‘’Watu wa mabara mengine wanaweza kupata chakula cha asili yao lakini pia sisi VETA-Mtwara tunafundisha jinsi ya kutengeneza vitafunwa pamoja na keki,biskuti,maandazi  na mikate zikiwemo keki zinazotokana na zao la Mwani”ameongeza Shirima

Gari za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Mtwara yanayotumika kufundishia wanafunzi wa kozi za udereva chuoni hapo kama yalivyokutwa na mpigapicha wetu Oktoba 28,2025.

Next Post
DCEA:Raia wa nchi jirani wanafadhili kilimo cha bangi Mara,yakamata tani 7.8

DCEA yamkamata ‘papa’ mwingine wa biashara ya dawa za kulevya

TFRA yapokea matokeo ya utafiti kuhusu uzalishaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini

TFRA yapokea matokeo ya utafiti kuhusu uzalishaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini

Maajabu kaburi la Chifu Manjonda linalopatikana katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia-Rondo

Maajabu kaburi la Chifu Manjonda linalopatikana katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia-Rondo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 8
  • Total visitors 13,064
  • Total page views 14,809

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In