• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, April 21, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Ujenzi jengo la Mahakama mkoani Njombe kutumia Sh.bilioni 7.2.

wananchi waelezwa kuwa Mahakama ndio sehemu pekee ambapo haki inapatikana

by bajeti
May 23, 2025
in Mazingira
0
Ujenzi jengo la Mahakama mkoani Njombe kutumia Sh.bilioni 7.2.

Jengo la kisasa la Mahakama mkoani Njombe linaloendelea kukamilika (Picha na Bajeti Communication)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MFAUME PASTORY,NJOMBE

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha huduma za Mahakama kwa ujenzi wa majengo bora ili kutoa haki kwa wananchi wanaofika kupata huduma za kisheria.

Majengo hayo yanayojumuisha Mahakama zote ikiwemo ya Rufaa ambayo baadhi ya mikoa yameshakamilika yanajumisha pia mifumo ya tehama ambapo pia husaidia kupunguza gharama kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo kwa kuzikutanisha mahakama zote katika jengo moja.

Mbali na baadhi ya mikoa mingine kukamilisha majengo hayo ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya za Temeke,na Ilala,Serikali sasa imetoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkoa wa Njombe

Bajeti Communication imefika katika eneo linakojengwa jengo hilo na kujionea hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wake likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika kwake.

Akizungunza na Bajeti Communication mkoani Njombe hivi karibuni,Mtendaji wa Mahakama ya Mkoa wa Njombe Richard Mbambe amesema kwa sasa Mahakama ipo katika maboresho mbalimbali ikiwa ni pamoja na majengo, usafiri, magari na mahakama mtandao.

Amesema pamoja na maboresho hayo lakini pia wanajenga  jengo la Mahakama Kuu Mkoa wa Njombe.

Ameongeza kuwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe walikuwa wanategemea Makao Makuu mkoani Iringa lakini kwa sasa hawataweza kwenda tena katika mkoa huo ila watahudumiwa mkoani Njombe.

”Hili litakuwa jengo jumuishi ambalo chini litakuwa na Mahakama ya Wilaya , katikati Mahakama ya Mkoa na juu Mahakama ya Rufani na litakuwa na lifti na inakadiriwa kugharimu kiasi cha Tsh.Bilioni 7.2” amesema Richard Mbambe.

Jengo la Mahakama mkoani Njombe likiwa katika hatua za mwisho kukamilika(Picha na Bajeti Communication)

Mbambe amebainisha kuwa ni jengo litakalokuwa na kila kitu ndani,ikiwemo mifumo ya kiteknolojia ambapo jengo kama hilo pia linajengwa katika mikoa ya Songwe na Singida.

Aidha amefafanuwa kuwa  wanaposema Jengo Jumuishi la Mahakama wanamaanisha kuwa  Mahakama zote ziko sehemu moja na mwananchi atapata haki zake katika jengo hilo.

Mbambe ameeleza kuwa kwa sasa elimu kuhusu Mahakama na utendaji wake imekua ikitolewa kwa wananchi hali iliyosaidia wananchi kunadai haki zao tofauti na zamani ambapo wananchi walitishiwa kwamba kuburuzwa Mahakamani hivyo kuogopa wakiamini kwamba wakipelekwa mahakamani basi moja kwa moja watakuwa na hatia.

“Lakini siku hizi watu wameelimika na hawaogopi kwenda mahakamani na kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kwenda kwenye kesi wakiamini kwamba mahakama ndicho chombo pekee kinachotenda haki.

“Kwa sasa Mahakama Mkoa wa Njombe inatekeleza Mradi huo mkubwa wa Mahakama Jumuishi, lakini kuna mradi wa Mahakama ulipo Lupembe  ambao umefikia asilimia 86 na mzabuni yuko njiani kuweka umeme na mradi mwingine ni upo Manda pamoja na Mradi wa lwilo ambao umekwisha kamilika na unatarajia kuanza kazi muda wowote”amebainisha Mbambe.

Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Njombe Richard Mbambe (kushoto) akizungumza na mwandishi wa habari na mwakilishi wa Bajeti Communication Nyanda za Juu Kusini Mfaume Pastory mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo Mbambe amewahimiza Wananchi mkoani Njombe kuwa  wanajukumu la kufahamu kuwa Mahakama  imejipanga kutoa haki kwa wakati hivyo wafike mahakamani wapate haki zao bila kuogopa kwa kuwa Mahakama ndio sehemu pekee ambapo haki inapatikana.

“Mahakamani ndipo mahala pekee ambapo haki inapatikana na elimu za kisheria hivyo wananchi wa Mkoa wa Njombe wanajukumu la kwenda kupeleka kesi zao ili haki ipatikane”ameongeza Mbambe

Next Post
Mgogoro wafukuta kiwanja kinachodaiwa kuwa cha shule Kigamboni

Mgogoro wafukuta kiwanja kinachodaiwa kuwa cha shule Kigamboni

Walinzi vituo mwendokasi ‘wasotea mishahara yao’,DART yakana kuhusika

Walinzi vituo mwendokasi ‘walilia mishahara’,DART yakana kuhusika

CUF yaomba Uchaguzi Mkuu kuwa huru,haki na amani

CUF yaomba Uchaguzi Mkuu kuwa huru,haki na amani

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:12
  • Today's page views 14
  • Total visitors 15,829
  • Total page views 17,939

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In