• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mgogoro wafukuta kiwanja kinachodaiwa kuwa cha shule Kigamboni

by bajeti
May 30, 2025
in Mazingira
0
Mgogoro wafukuta kiwanja kinachodaiwa kuwa cha shule Kigamboni

Eneo llinalopakana na Shule ya Sekondari Minazini iliyopo Mtaa wa Mkwajuni Kata ya Vijibweni, Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ambalo linaelezwa kuwa ni shule lakini pia linadaiwa kumilikiwa na Mohamed Chande

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU.

MIGORORO ya ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea kuwa jinamizi lililoshindikana ambapo baadhi ya maeneo ya shule na viwanja vya wazi vimeingia katika migogoro hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na Bajeti Communication umebaini hivi karibuni kuwapo kwa mgogoro katika eneo la Shule ya Sekondari Minazini iliyopo Mtaa wa Mkwajuni Kata ya Vijibweni, Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Hata hivyo baadhi ya viongozi waadilifu ndani ya Serikali ikiwemo mtaa na kata, wamekuwa kikwazo kwa wahusika kufanikisha azma yao ya kulichukua na kuliuza eneo hilo.

Akizungumza na Bajeti Communication, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale amesema alitoa maelekezo mnamo April 10, 2025 juu ya eneo hilo kuwekewa vibao kuonyesha ni mali ya shule, lakini siku iliyofuata  viling’olewa.

“Aliyefanya tukio lile la kung’oa vibao mpaka sasa tunamtafuta, hatujampata,kitendo kile ni kosa la jinai, tukimnasa tutamchukulia hatua za kisheria,” amesema Kiwale.

Wakati Mkurudgenzi Kiwale akieleza hivyo, Mkazi wa Rufiji mkoani Pwani, anayedai kulimiliki eneo hilo, Chande Mohamed Chande (76) amekiri kuwa ndiye anayemiliki eneo hilo  na kwamba vibao vinavyoelezwa kuwekwa katika eneo hilo havikuwa vimewekwa kwa amri ya Mkurugenzi Manispaa ya Kigamboni.

“Vibao vya shule vilivyotolewa vimetolewa  kwenye eneo langu, aliyeviweka kwanini aviweke usiku?

“Eneo lote la wazi ambalo halina uzio takribani ekari moja na nusu ni langu, wanaotaka kunipora ardhi yangu wanatumia kigezo kwamba nasingizia sijalipwa fidia ya mwanzo.

“Malalamiko yangu si fidia, ni eneo langu ambalo shule wamechukua kinguvu na kudai ni lao ilhali si kweli,” amesema Chande.

Aidha amebainisha kuwa baada ya kupimwa kwa maeneo ya shule,yaliwekewa uzio ambao hata hivyo ulichakaa miaka ya nyuma na kuwekwa mwingine kwa kuzingatia mpaka wa awali ulikopitishwa.

“Ni kwanini baada ya kujenga uzio mpya wa sasa, shule imeendelea kuzingatia mipaka ya zamani badala ya kulizungushia eneo lote tena katika kipindi cha sasa ambacho lina mgogoro”anabainisha Chande

Chande ameongeza kuwa chanzo cha eneo hilo kupokwa mikononi mwake ni baada ya kupata matatizo ya kiafya ukiwamo ugonjwa wa kupofuka macho na baada ya kupona aliamua kuhama Kigamboni na kwenda kuishi Rufiji mkoani Pwani.

“Nikiwa Rufiji wakaanza kulifanyia mpango wa kulichukua wakidai serikali ililichukulia pamoja na maeneo mengine yaliyotolewa fidia, walidai ni la kufanyia michezo na mikutano, wakati huo mimi sikushirikishwa hata kidogo,” amesema Chande.

Hata hivyo Chande, amebainisha kuwa amehangaika kurejesha eneo hilo mikononi mwake zaidi ya miaka mitatu sasa na kwamba amefika hadi ngazi ya Manispaa lakini hajafanikiwa huku akisisitiza kuwa Serikali ya Mtaa na Kata hawajawahi kupinga kuwa si mali yake.

“Majirani wote wanaoishi karibu na eneo lile ukiwauliza watakueleza kuwa mimi nimelima pale, hakuna atakayekuthibitishia kuwa mimi natumika kufanya utapeli,mimi na uzee wangu huu?” ameeleza Chande.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkwajuni, Tatu Kondo,amesema katika eneo hilo hakuwahi kuona vibao wala kupewa taarifa kama vimewekwa.

“Kwanza mimi ni mpya kwenye uongozi, sifahamu chochote kuhusu hayo malalamiko, wala sina taarifa kwamba kuna watu hawakufidiwa,” anmesema Kondo.

Mmoja wa walimu wanaofundisha shuleni hapo ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi, amesema eneo hilo ni mali ya shule na kwamba hakuna mgogoro wowote kwenye eneo hilo.

“Labda nachoweza kueleza hapa ni kwamba Machi 27, 2023 kuna watu wa Manispaa walifika kwenye lile eneo na kuanza kufanya upimaji bila sisi kuwa na taarifa, tulitaharuki. Tulipowahoji, wakadai wametumwa na Mkurugenzi.

“Hatukuridhishwa na majibu yao tukalazimika kuandika barua kwa Mtendaji Kata ili kujua ujio wao kama una baraka za ofisi yake, Ilibidi kesho yake Mtendaji aitishe kikao, kwenye kikao kile tukaelezwa kuwa Mzee Chande ndiye amepeleka barua katani hapo akidai kuwa eneo ni mali yake,” amesema Mwalimu huyo.amese mwalimu huyo

Kutokana na madai ya Mzee Chande, anasema uongozi wa shule ulifikisha taarifa kwa DED, akalazimika kuitembelea shule hiyo na kufanya ukaguzi wa mipaka ya eneo na mara baada ya ukaguzi akatamka wazi kuwa ni mali ya shule.

[custom_chatbot]

 

Next Post
Walinzi vituo mwendokasi ‘wasotea mishahara yao’,DART yakana kuhusika

Walinzi vituo mwendokasi ‘walilia mishahara’,DART yakana kuhusika

CUF yaomba Uchaguzi Mkuu kuwa huru,haki na amani

CUF yaomba Uchaguzi Mkuu kuwa huru,haki na amani

ZAFICO yatambulisha ufugaji wa samaki wa vizimba

ZAFICO yatambulisha ufugaji wa samaki wa vizimba

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In