• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

AAFP  kujenga ukuta mipaka yote ya Tanzania

Kulifuta Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),kuanzisha Jeshi la Ulinzi na Vita

by bajeti
September 25, 2025
in Siasa
0
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Wakulima(Alliance for Africa farmers Party -AAFP) kimesema Serikali yake itajenga ukuta kuzunguka mipaka yote kutokana na nchi jirani na duniani kuwa na vurugu

Hayo yataekelezwa ikiwa chama chao kitapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kuongoza dola katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025.

Hata hivyo licha ya kujenga ukuta katika mipaka yote ya nchi,Serikali ya AAFP italifuta Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na badala yake kuwa na Jeshi la Ulinzi na Vita na Jeshi la Maendeleo Tanzania.

Hayo yamebainika katika Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho katika kipindi cha 2025-2030 yenye kauli mbiu  “Mabadiliko ni Lazima”

Ilani hiyo ya mabadiliko ya (AAFP) (chama cha wakulima) 2025 – 2030 iliandaliwa na kupitishwa na Kikao cha Kamati Kuu cha Aprili 27,2025 na kupata baraka ya Mkutano Mkuu wa Aprili 29,2025 jijini Dar es salaam ambayo itaanza kutumika rasmi kwanzia 2025 – 2030.

AAFP inayoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa  Saidi Sudi Saidi na Katibu Mkuu  Rashid Rai kupitia Ilani  ya chama hicho inaitaka Serikali yake kuzungusha ukuta katika mipaka ya nchi nzima

Hata hivyo Ilani hiyo imebaisha kuwa kwa kuwa nchi nyingi za majirani na duniani kote kumekuwa na migogoro au vurugu za kidiplomasia, hivyo Ilani ya chama chao  cha AAFP inaitaka Serikali ya yake ifanye mambo yafuatayo

”Kutengeneza vinu vya nyukilia ,Kutengeza ndege zisizo na rubani (Drone)  na kuzungusha ukuta kwenye mipaka ya nchi nzima”

“Kwa kuwa wananchi wanauhitaji wa suala la uraia pacha, hivyo Ilani ya chama chetu cha AAFP inaitaka Serikali  yake kutengeneza sheria ya namna bora ya watu kupata uraia pacha”imeeleza Ilani hiyo

Kwa upande wa masuala ya Ulinzi na Usalama,AAFP kupitia Ilani yake kinakusudia kufanya mabadiliko makubwa katika majeshi nchini ambapo Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), litagawanywa katika makundi makubwa mawili ambalo ni Jeshi la Ulinzi na Vita na Jeshi la Maendeleo Tanzania

“AAFP inakusaidia kufanya mabadiliko makubwa katika majeshi yetu nchini ambapo Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), litagawanywa katika makundi makubwa mawili ambalo ni Jeshi la ulinzi na vita,likiwa na  kazi za ulinzi wa mipaka ya nchi na mambo ya vita.

“Wataalamu wote wa mambo ya kivita na ulinzi wa mipako ya nchi watajiunga katika jeshi la ulinzi na vita ambalo litaitwa (jeshi namba moja na Jeshi la Maendeleo Tanzania

“Sera inakusudia serikali kuweka utaratibu wa kisheri kwamba kazi na miradi yote ya maendeleo ndani ya nchi kama vile (kandarasi) ya Ujenzi wa Barabara, Majengo, utengenezaji wa Madawati, na miradi yote kama hiyo inatekelezwa kwa kufanywa na kusimamiwa na jeshi maalum la maendeleo”imebainisha Ilani hiyo

Ilani hiyo imebainisha kuwa Wataalamu wote wa jeshi kwa viwango tofauti watajiunga katika Jeshi la Maendeleo ili kuhakikisha kwamba wanakomesha wizi uliozoeleka katika kutekeleza miradi ya maendeleo

“ Ilani inakusudia kuweka nidhamu katika shughuli za maendeleo na pia kuongeza Ajira kwa vijana.

“Kwa muktadha huo, Jeshi la kujenga Taifa JKT linafutwa na kuchanganywa katika Jeshi la Maendeleo Tanzania ambalo litaitwa ‘’Jeshi namba mbili’’.

Kwa upande wa Idara ya usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Magereza, Zima Moto, Uhamiaji na idara zingine kama hizo zitabaki kuwa zilivyo au zitafanyiwa mabadiliko pale itakapohitajika.

Alliance for Africa farmers Party (AAFP) (Chama cha Wakulima) kilipata usajili wake kamili Novemba 3, 2009 kwa jina la Alliance for Tanzania farmers party (AFP) (chama cha wakulima).

Aidha Februari 10,2018 katika Mkutano Mkuu wa pili wa chama hicho walipitisha Azimio la kufanya marekebisho machache katika katiba ya (AFP) ya mwaka 2009 na kubadili jina na sasa Alliance for Africa farmers party (AAFP) (chama cha wakulima) chini ya katiba mpya ya (AAFP) ya mwaka2009 – 2018.

Watanzania wanatajia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025 kuwachagua Rais,Wabunge na Madiwani ambapo vyama 18 vinashiriki katika uchaguzi huo.

Next Post
TRA yahimiza ulipaji wa kodi kwa hiari

TRA yahimiza ulipaji wa kodi kwa hiari

CHAUMMA:Hatma ya maisha ya watanzania ni Oktoba 29,2025

CHAUMMA yataka mfumo wa serikali tatu

CCM kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya

CCM kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 16,472
  • Total page views 18,683

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In