• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, July 11, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Kuelekea Dira ya Maendeleo 2050,Kuku wa nyama kuuzwa kwa uzito(kilo),’wafugaji wanukia utajiri’

COSTECH yatajwa kwa ufadhili

by bajeti
June 18, 2026
in Sayansi na Teknolojia
0
Kuelekea Dira ya Maendeleo 2050,Kuku wa nyama kuuzwa kwa uzito(kilo),’wafugaji wanukia utajiri’

Kuku wa nyama sasa kuuzwa kwa kila na si kwa namba kama ilivyozoeleka kwa wanunuzi

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

TANZANIA inatajwa kuwa na jumla ya kuku milioni 87.7 huku wakulima wadogo wakiwa na kuku milioni 75.1 na mashamba makubwa yakiwa na kuku milioni 12.5.

Hayo ni kwa mujibu wa  Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Ripoti hiyo imeonesha kuwa idadi ya kuku waliofugwa nchini ni walikuwa ni Milioni 87,6 ambapo Tanzania Bara walikuwa Milioni 83.8 na upande wa Zanzibar kulikuwa na Kuku Milioni 3.7.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Idara ya Uzalishaji na Masoko katika Mashamba ya Kuzalisha Mifugo inaeleza kuwa kuku wa kisasa wanafikia milioni 44.5 huku kuku wa asili wakifikia milioni 38.77 ambapo Sekta ya Mifugo ilikuwa kwa asilimia tano katika mwaka 2019/2020.

Sensa hiyo inaonesha uhalisia wa wafugaji wadogo jinsi walivyo wengi ikilinganishwa na wafugaji wenye mashamba makubwa.

Hata hivyo imezoeleka kwa wanunuzi wa kuku kuwanunua kwa makundi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzito mdogo na gharama kubwa ya kuwalisha ikiwemo chanjo jambo linalowagharimu sana wafugaji.

Mbali na hilo lakni pia wakulima wengi hawajidhatiti katika kuangalia ubora wa nyama ya ndege hao ili kufikia viwango vya kimataifa na kujiingiza katika masoko ya nje na kujiongezea kipato chao mwenyewe na Taifa kwa ujumla.

Wakati wafugaji wakikata tamaa ya ufugaji wa kuku hasa wa nyama kutokana na gharama kubwa za chakula ikiwemo chanjo na faida kidogo inayowapelekea kuwauza kama vifaranga,chakula cha ndege hao wa nyama wanaotajwa kuwa wenye protini nyingi katika mwili wa binadamu kimepatikana.

Mbali na gharama za chakula kuwa juu cha ndege hao wa nyama lakini pia  wanahitaji chanjo ya kuwakinga na magonjwa mbalimbali ili waweze kukua jambo ambalo pia linaongeza gharama kubwa kwa wakulima na kuwafanya kukata tamaa ya kuwafuga.

Kwa kuthibitisha gharama za chakula na chanjo zinazohitajika kwa ndege hao,Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha kuwa idadi ya kuku waliochanjwa waliofikia asilimia 50.

Katika Sensa hiyo iliyohusisha aina mbalimbali za mifugo iliyofugwa nchini wakiemo Ngo’mbe,Mbuzi,Kondoo,Nguruwe na Kuku imeonesha idadi ya kuku waliochanjwa nchini.

“Idadi ya Kuku waliochanjwa nchini kwa upande wa ugonjwa na Mdondo/Mhepe ni 44,591,494 sawa na asilimia 50.9 ambapo kwa upande wa ugonjwa wa Gumboro walichanjwa kuku 9,903,930  na ugonjwa wa Ndui wakiwa Kuku 13,560,766

“Ugonjwa wa mdondo/mhepe ulichanjwa kwa kiwango cha juu zaidi cha asilimia 50.9 na Gumboro kwa kiwango cha chini zaidi cha asilimia 11.3 ya kuku wote waliofugwa na wakulima wadogo”imebainisha ripoti hiyo

Hata hivyo ripoti hiyo imefafanuwa kuwa kwa upande wa Tanzania Bara,Kuku waliopata chanjo  kwa ugonjwa wa Mdondo/Mhepe walikuwa Milioni 43.7 sawa na asilimia 52.2 ambapo Gumboro wakiwa ni Milioni 9.4 sawa na asilimia 11.2 huku ugonjwa wa Ndui wakiwa ni Milioni 13.1 ikiwa ni sawa na asilimia 15.7.

“Tanzania Zanzibar Kuku waliochanjwa ugonjwa wa Mdondo/Mhepe walikuwa ni 796,209 sawa na asilimia 21.2,Gumboro  501,821 ikiwa ni sawa na asilimia 13.3,na Ndui wakiwa 422,457 sawa na asilimia 11.2”imeongeza ripoti hiyo

Kutokana na tafiti na ripoti mbalimbali zinazoonesha uthibitisho wa mahitaji ya chakula na chanjo kwa ndege hao na idadi kubwa ya wakulima wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku kulikuwa na ombwe kubwa la kupatikana kwa chakula kisichotumia kemikali na kusaidia kuku hao kuondokana na chanjo kama wanavyotibiwa binadamu ili hali wanatumika kama kitoweo.

Hata hivyo kilio hicho cha wakulima kinaelekea mwisho baada ya mtanzania kutafiti na kubuni chakula cha kuku wa nyama kisicho na kemikali lakini pia chenye kinga kinachozalishwa kwa malighafi za asili lakini vilivyochanganywa kisayansi.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki sababu na nia ya uzalishaji wa bidhaa hiyo,Mbunifu wa chakula hicho Whitefrank Frank anasema wao wamekuja na bidhaa ya chakula cha kuku wa nyama pekee ambacho kimezaliwa kutokana na tafiti na bunifu za vijana wa kitanzania.

Anasema wao wanatoka katika familia za wakulima na wanafahamu vizuri kuhusu suala la ufugaji wa kuku kuanzia kuku wa kienyeji hadi wa kisasa ambao ni nyama pamoja na mayai.

“Changamoto kubwa ambayo wakulima wamekuwa wakiipitia ni gharama kubwa za ufugaji nikiwa namaanisha gharama za mkulima kutoka ananunua kifaranga mpaka kumtoa kuku na kufikia wa nyama au kutaga mayai.

“Sehemu kubwa ya gharama imekuwa upande wa chakula na madawa nikimaanisha chanjo  na vingine.

“Sisi tukaona tunaweza tukafanya kitu upande wa chakula cha kuku hasa kitu kinachosababisha chakula cha kuku wa nyama kiwe na gharama ya juu kiasi wakati mwingine kinamshinda mkulima wa kawaida anaishia kutumia vyakula vya kuchanganya tu kawaida mtaani”anasema Frank

Aidha anabainisha kuwa baada ya kuona hilo waliamua kutengeneza mfumo wenye vipengele vitatu ili kutatua changamoto hiyo kwa wakulima ambapo kwanza waliangalia namna ya kuongeza uzito wa kuku wa nyama ndani ya muda mfupi,pili kuzalisha kwa gharama ndogo na tatu kutumia malighafi inayopatikana katika mazingira yao kama mimea,wadudu,mahindi na vingine na kuviingiza ili kuunda mfumo mmoja.

Anaeleza kuwa baada ya kutengeneza mfumo huo wa kwanza ,waliweza kupata “support” kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH)   na wakapata mtaji mbegu wa kwanza (Seed Fund) akimaanisha  kuwa “una wazo ambalo bado halijakaa sawa na unapewa ile fedha ukahakiki lile wazo na baadaye lifae kuwa biashara”.

“Tukapata dola 5700 na baada ya hapo tukafanya ushirikiano na watalaam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA) na tukaenda kuhakiki mfumo wetu kama unaweza kuleta matokeo.

“Tuliweka vifaranga wengi wa kuku wa nyama kama 800 na tukafanya uhakiki wetu  na matokea tuliyapata kwamba tumetengeneza chakula cha kuku ambacho kimeletea hayo matokeo.

“Kuku wa nyama(broiler) anaweza kufikia kilogram 1.5 au kilo mbili ndani ya muda mfupi wa wiki tatu hadi nne lakini pia  chakula kinapatikana chini ya asilimia 20 ya bei inayouzwa sasa hivi”anasema Frank

Frank anaeleza kuwa hicho chakula kinamsaidia kuku wa nyama kupata kinga ya mwili ya kawaida hivyo kupunguza gharama ambayo mkulima anaingia kwa ajili ya dawa.

“Mfumo wote uliotumika kutengeneza chakula hiki hakuna kemikali ambayo tunaiongeza zaidi ya organic katika hizi formuler yetu ya kutengeneza chakula.

“Baada ya hapo tukaenda kuhakiki jambo hilo kwa wakulima  wakiwemo wa Mkoa    wa Morogoro katika mazingira yao ya nyumbani kwa kutumia chakula hicho na matokeo yamepatikana na baada ya kufanya majaribio sasa tukawa tayari kwa ajili kufanya biashara ya chakula cha kuku kinachotengenezwa kwa malighafi za kiasili lakini zenye matokeo bora”anabainisha Frank

Frank anaeleza kuwa  walifanya utafiti wao kwa wiki sita na walikuwa na kuku waliofikisha uzito wa kilo tatu  mbali na wale waliofikisha wiki tatu wakiwa na uzito wa kilo moja na nusu hadi mbili

“Jambo lingine tuliloligundua katika ufatiti wetu ni kwamba kuna changamoto kubwa kwa wakulima wetu kufuata kanuni  bora za ufugaji wa kuku ikiwemo kulinda kuku na mambo ya vimelea(by security),kusafisha na mengine ambayo inachangia kuleta matokeo.

“Tukapokwenda sokoni pia utakuwa ni utamaduni wetu kuwaelimisha wakulima kuhusu hilo suala kwani pia linachangia kuhusu matokeo”anafafanuwa Frank

Kuku wa nyama akipimwa kwa kilo baada ya kulishwa chakula cha kisasa.

Aidha anabainisha  kuwa kuku wa nyama ana hatua katika ukuaji wake na wao wametengeneza chakula hicho kwa kila hatua ili kutoa matokeo bora kwa mkulima na kumuinua kiuchumi ambapo kila hatua kinahitajika chakula chenye mfumo tofauti ambapo akiwa kwenye kifaranga anahitaji kuwa na chanjo.

Akizungummzia kuhusu majaribio ya chakula hicho,Frank anasema kuwa mchakato wa kukijaribu chakula hicho kilihusisha awamu mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni ya kisayansi yaani kukipima kwa mfumo wa kutumia methodology, treatment  kisayansi lakini pia baada ya hapo waliangalia ikiwa wao wamemefanya kisayansi sana na wakulima wanaweza wasifanye hivyo, hivyo wakaona pia kujaribu katika mazingira halisi kwa wakulima ambao hawatafanya kisayansi  na matokeo yalikuja sawa na yale ya kisayansi.

Kuku wa nyama

Frank anabainisha kuwa chakula hicho ni kwa ajili ya kuku wa nyama pekee lakini pia haimaanishi kuwa watajikita huko pekee kwani wanachotaka kufanya ni kutengeneza utamaduni wa kufanya vitu kwa tafiti na ndio sababu ya kutokimbilia kuingia sokoni na walitangulia kwanza kwenda maabara ili kitu chao watakachokipeleka sokoni kinafaa kwa kiasi gani.

“Huu ndio utakuwa utamaduni wetu,tutakapotaka kutengeneza bidhaa za kuku wa mayai,samaki na wanyama wengine tutatumia kama tulivyofanya hii kwa kufanya tafiti na tutakuja na kitu ambacho kimethibitishwa kisayansi”anaeleza Frank

Faida kwa wakulima

Akizungumzia kuhusu faida watakazopata wakulima baada ya bidhaa kuingia sokoni,Frank anasema wakulima watapata faida kubwa ikiwemo mkulima kukaa na kuku kwa siku nyingi ikiwasubiri wakue ndipo awauze.

“Nafikiri wakulima watapata faida,tunakwenda kupunguza mzunguko wa mkulima kukaa na kuku kutoka wiki nne hadi wiki tatu lakini pia tunakwenda kumsaidia mkulima afikie uzito kamili wa kilo moja na nusu hadi kilo mbili.

“Ninafahamu kwamba changamoto iliyopo kwa wakulima sasa hivi huenda ikawa changamoto ya kisera,broiler wanauzwa kwa namba,nikimaanisha leo ukiwa na kuku wako unataka kuwauza ukimleta tajiri anawahesabu kuanzi moja  na kuendelea na kisha anakupa bei moja.

“lakini sasa hivi hata Serikali inataka kuona kuku anauzwa kwa uzito  na hiyo ndio itakuja kumletea faida zaidi mkulima  na itaongeza wale ambao wanafanya mauzo ya chakula cha mifugo kufikiria sasa kuanza kufanya tafiti na bunifu ili kumsaidia mkulima kupata uzito unaostahili  na wenye faida”anasema Frank

Hata hivyo Frank anaeleza kuwa kwa sasa kila kitu kipo sawa na wanaendelea na ushirikiano na COSTECH ili bidhaa hiyo iweze kuingia sokoni kwa haraka iwezekanvyo na itakapokuwa tayari basi pia watahitaji vyombo vya habari ili viweze kuwajulisha wananchi kuhusu uwepo wa bidhaa hiyo muhimu kwa chakula cha kuku wa nyama

 

 

Ushindani wa soko

Akizungumzia kuhusu ushindani wa soko la bidhaa hiyo,Frank anakiri kuwa ushindani ni mkubwa lakini anasema katika taarifa iliyotolewa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Nethaland umeonesha kuwa kuna wazalishaji wengi wa chakula cha kuku nchini lakini bado hawakidhiti mahitajimya wakulima.

“Watu wapo ambao wanazalisha chakula cha kuku lakini naweza kukwambia kwamba mahitahji ya chakula cha kuku ni asilimia 40 ndio inayopatikana na hiyo  ndio inayopelekea bei kuwa juu na asilimia 60 ya chakula cha kuku bado kinahitajika.

“Sisi tutakachoenda kukifanya, tutatumia ‘Blue Market Strategic’,tutaenda kulichukua soko hili ambalo bado halijafikiwa la asilimia 60 lakini pia tuna watu wengi ambao hawajaingia kwenye shughuli za ufugaji wa kuku na changamoto kubwa ni mitaji kwa sababu ya gharama za uendeshaji.

“Kwa kutumia mbinu hii tutawavutia watu wengi zaidi kuingia,pamoja na kwamba mtaani ushindani ni mkubwa,keki bado ipo na hawa waliopo bado hawajaweza kuifikia yote.anaongeza Frank

Frank anaeleza  kuwa kwa kuanza wataanzia Mkoa wa Dar es Salaam,Pwani na Morogoro  na baadaye wataelekea Kanda ya Kati katika mikoa ya Singida na Dodoma na awamu ya tatu watakwenda Kaskazini katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Chakula cha kuongeza uzito wa kuku kinachozalishwa na Whitefrank Frank

Mkono wa Serikali katika kuthibitisha tafiti na bunifu za kisayansi

Akizungumzia kuhusu Serikali kushiriki katika uhakiki wa utafiti na bunifu za kisayansi,Frank anabainisha kuwa Serikali ina miongozo ya kuthibitisha tafiti hizo na bunifu kwa kuweka vigezo vitakavyoondoa mashaka juu ya bidhaa zitakazozalishwa na watafiti.

“Serikali yetu kupitia taasisi zake inamuongozo na wanakwambia wewe fanya chochote lakini tunahitaji tukienda kupima tukute mfano wanga kiasi hiki,protini kiasi hiki tuone vitu hivyo na vingine vikienda kwenye nguvu vinaleta hivi,hivyo ni vitu ambavyo vinafanyika kisayansi.

“Kabla ya kupelekea bidhaa sokoni unahitajika kwenda kwenye Mamlaka za Serikali kuhakiki hivyo vitu kama kweli vipo,lakini ni bahati mbaya tu kwamba bado tuna watu ambao wanafanya biashara bila kupitia mchakato huo,Serikali ina Sera nzuri tu kwenye hilo suala na muhimu sana kama utatoa chakula nje lazima wakihakiki na kama wao watakuwa wamehakiki basi kitakuwa kimefikia viwango.anafafanuwa Frank

Azungumzia dhana ya ulaji kuku wa kisasa na afya ya binadamu

Akizungumzia kuhusu kula mifupa na nyama ya kuku kuathiri afya ya binadamu kutokanana kile kinachoelezwa kuwa ukuaji wa ndege hao hutegemea dawa za kemikali,Frank anasema anaelewa kasumba hiyo iliyopo mtaani na nyingine sio kasumba bali uthibitisho wa kisayansi kuwa kuku wa kisasa walikuwa na kiwango kikubwa cha Untibiotics na vingine lakini kwa upande mwingine ni kwamba broiler ni chanzo kikubwa cha protini.

“Sisi Tanzania tunachangamoto ya ukosefu huo wa protini lakini unaweza usilione hilo lakini mkifuatilia mtaona tuna shida kubwa ya utapiamlo,ukosefu wa protini kwa hiyo kwangu mimi ni kwamba bado ni muumini mkubwa kuwasukuma wakulima wengi kujiingiza kwenye ufugajiu wa kuku wa nyama.

“Tungependa kuona nyumba moja moja inakuwa na access na chanzo cha kuaminika cha protini ,lakini pili tutaweza kuongeza vipato vyao.

“Changamoto zipo kwa baadhi ya wakulima wenye hizo kasumba na kuaminishwa wakiwakilisha kuku hiki kitakuwa hivi na wakifanya hivi itakuwa hivi,lakini sasa ni suala la vyombo vya habari kwenda kuelemisha jamii kuwa hauhitaji kumlisha kuku chakula hiki bali unahitaji kumlisha chakula bora ambacho hakina kemikali na unahitaji kufuata kanuni bora ambavyo vinatosha kabisa kukupa uzito unahitajika sokoni.anasema Frank

Aidha anongeza kuwa chakula bora ambacho hakina kemikali na kufuata kanuni bora za ufugaji vinatosha kabisa kukutengenezea nyama bora ya kuku na kuuza hata kwenye masoko ya nje

Mbunifu wa chakula hicho Whitefrank Frank

Utafiti wake na Dira ya Maendeleo 2050

Akizungumzia kuhusu utafiti na ubunifu wake wa chakula cha kuku wa nyama na Dira ya Maendeleo 2050,Frank anafafanuwa kuwa Dira ya Maendeleo 2050 inatakuwa kuwa na uchumi unaofikia Sh.Trilioni moja  sasa hadi sasa kuna miaka 25 ya kutekeleza suala hilo.

“Asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira hiyo,Serikali inasema itatekelezwa na Sekta Binafsi na asilimia zingine ni kwenye makampuni binafsi.

“Sasa asilimia 70 kutekelezwa na Sekta Binafsi tunahitaji vitu vitatu,kwanza tunahitaji Sekta Binafsi ambayo ina mtaji lakini pia Sekta Binafsi ambayo itaendeshwa na ubunifu lakini pia tutahitaji Sekta Binafsi ambayo itagusa mahitaji ya moja kwa moja ya watu wetu”anasema Frank

Frank anabainisha  kuwa wao kwa utafiti na ubunifu wao watakwenda kwenye Sekta ya Kilimo ambapo asilimia 70 watu wameajiriwa huko hivyo watakwenda kusaidia wakulima wadogo na wa kati kuweza  kuongeza faida.

“Hii nyongeza tunayoipeleka kwenye Sekta ya Kilimo na nyongeza pia kama Sekta Binafsi naamini kwa kiasi kikubwa tutachangia kwenye mchakato mzima kwenda kwenye Dira yetu ya  Taifa ya Maendeleo 2050.”anabainisha Frank

Kuku wa nyama akipimwa uzito

 Aishukuru COSTECH

Katika hatua nyingine Frank ameishukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia katika mchango wake mkubwa wa kuwasaidia watafiti na wabunifu ili kufikia hatua za uzalishaji  bidhaa katika kutatua changamoto kwa wananchi.

“ Tulifanya kazi hii kupitia fedha kutoka serikalini kupitia COSTECH na Wizara ya Elimu katika shindano la MAKISATU wameshafanya sehemu na hii ya pili nawasihi sana tuendelee kuhakikisha kwamba hii bidhaa inaingia sokoni kwa kadri inavyowezezekana.

“Watu ambao watahitaji kuzungumza na sisi,tupo katika Kituo Atamizi (DTI)kilichopo chini ya COSTECH  kwa ajili ya kuatamiza wabunifu na hapo ndio tunahitaji wale ambao watahitaji kuisaidia  COSTECH ili kuipelekea bidhaa sokoni wanawakaribisha”anasema Frank

Wawekezaji wakaribishwa

Hata hivyo Frank amewakaribisha watu wote ambao wanahitaji kuwekeza katika ubunifu wao na kuingia sokoni kwa kufanya kazi nao wako tayari.

Wakulima watoa ya motoni

Wakizungumzia ujio wa bidhaa hiyo,baadhi ya wakulima wamesema ni muhimu kwa tafiti na bunifu zinazoanzishwa na watanzania kuendelezwa kwa sababu wao ndio wanaojua matatizo yanayowasibu lakini sio za kutoka nje ya nchi.

“Mtanzania akifanya utafiti na ukathibitishwa na vyombo husika basi ni muhimu Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo hiyo uliyoniambia ya COSTECH kuhakikisha kuwa tafiti na ubunifu huo unazalisha bidhaa kwa ajili ya matumizi ya watanzania kwa kuwa wao ni miongoni mwa jamii zinazoishi na kukulia hapa hivyo mbali na tafiti lakini pia wameziishi changamoto hizo kiuhalisia.

“Mimi nilikuwa nafuga kuku lakini naleta vifaranga 200 vinavyokuwa hadi kuviuza ni 60 hadi 80 vingine vyote vinakufa na ukiuliza sababu utaambiwa hukuwapa  chanjo au walikuwa na ugonjwa sasa inatupa shida kwani un akuwa umeshapoteza mtaji kutoka kuku 200 hadi 80 wengine waliokufa wanafidiwa na nini”amesema Boniface Mohamed mfugaji wa kuku kutoka Chanika jijini Dar es Salaam.

Naye Mariam Salehe kutoka Kitunda jijini Dar es Salaam anasema wanasubiri chakula hicho waone ikiwa kitawasaidia kwani lengo la kufuga ni kuinuka kiuchumi lakini hasara ni kubwa kuliko faida kwani wakati mwingine wanauza kuku hao wakiwa na wiki mbili na nusu ili kuepuka gharama na wao kupata faida japo ni kidogo.

Salehe ameishauri Serikali kuongeza fedha katika kuendeleza tafiti na bunifu hizo kwani zimekuwa na majibu kwa changamoto zinazowahusu watanzania hivyo kupunguza utegemezi wa utaalamu kutoka mataifa ya nje.

Next Post
JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Migongano baina ya binadamu na wanyamapori ni tishio kwa uhifadhi  endelevu

Matukio 1718 ya milipuko na moto hayajachunguzwa

Wajumbe wenye elimu darasa la saba wabainika Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tukuyu

Kutoka takaozo hadi uzalishaji wa chakula cha wanyama  kupitia Nzi Chuma

Kutoka takaozo hadi uzalishaji wa chakula cha wanyama  kupitia Nzi Chuma

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:122
  • Today's page views 122
  • Total visitors 20,836
  • Total page views 23,210

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In