• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, July 10, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Migongano baina ya binadamu na wanyamapori ni tishio kwa uhifadhi  endelevu

Migongano 1995 yasajiliwa,Hifadhi ya Nyerere yaongoza 

by bajeti
June 22, 2026
in Mazingira
0
JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Tembo wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere amebaini kuwepo kwa migongano zaidi ya 1900 baina ya binadamu na wanyamapori iliyosababisha mauaji na uharibifu wa mali.

CAG Kichere ameyabainisha hayo katika Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 iliyotolewa tarehe 30/3/2026 .

Amesema katika mapitio yake ya Ripoti ya Utekelezaji wa Sheria za wanyamapori ya mwaka 2024/25 katika hifadhi 10 za Taifa, yamebaini matukio 1,783 ya migongano kati ya binadamu na wanyamapori.

“Migongano hii inahusu muingiliano kati ya watu na wanyamapori ambao unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo, lakini si tu, ushindani wa rasilimali chache unaosababisha madhara kwa binadamu na wanyamapori”amesema CAG Kichere

Amesema  migongano kati ya binadamu na wanyamapori ni moja ya tishio kuu kwa uhifadhi endelevu na ustawi wa watu wanaoishi jirani na maeneo yaliyohifadhiwa (madhara hayo ni pamoja na wanyama kuvamia mashamba, kuua binadamu, na kuharibu mali kama vile mashamba na mazao katika vijiji.

“Katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, migongano kati ya binadamu na wanyamapori iliyosajiliwa ilikuwa jumla 400.

“Matukio haya yalisababisha vifo vya wanyamapori , uharibifu wa mazao, uharibifu wa mali, majeraha, na vifo”ameongeza CAG Kichere

CAG Kichere amefafanuwa kuwa migogoro hiyo kati ya binadamu na wanyamapori ilisababishwa na shughuli za kibinadamu ndani ya mipaka ya maeneo ya hifadhi na  kutokuwapo kwa vizuizi ili kuzuia wanyamapori kuvamia maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa wanyamapori na binadamu.

“Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ilikuwa na idadi ya visa 512  katika vijiji 61,Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ilikuwa na idadi ya visa 377 katika  vijiji  43 ,Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ilikuwa na idadi ya visa 55 katika  vijiji vinne,Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilikuwa na  idadi ya visa 221  katika vijiji 18 ,Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilikuwa na idadi ya visa 272  katika vijiji 27,Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ilikuwa na  idadi ya visa 29  katika vijiji 13 ,Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  ilikuwa na idadi ya visa 73  katika vijiji 12 ,Hifadhi ya Taifa ya Katavi  ilikuwa na idadi ya visa 61 katika  vijiji tisa,Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara ilikuwa na idadi ya visa  59 katika vijiji 38 na Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilikuwa na idadi ya visa124  katika vijiji 12.

“Jumla  idadi ya visa ilikuwa 1,783  na vijiji 237 ,Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro ilikuwa na idadi ya visa 212 katika vijiji 35,jumla kuu ni idadi ya visa  1,995  na vijiji 272.”ameongeza CAG Kichere

Next Post
Matukio 1718 ya milipuko na moto hayajachunguzwa

Wajumbe wenye elimu darasa la saba wabainika Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tukuyu

Kutoka takaozo hadi uzalishaji wa chakula cha wanyama  kupitia Nzi Chuma

Kutoka takaozo hadi uzalishaji wa chakula cha wanyama  kupitia Nzi Chuma

Uzalishaji juisi ya ndizi utakavyoongeza  ajira,soko la uhakika kwa wakulima

Uzalishaji juisi ya ndizi utakavyoongeza ajira,soko la uhakika kwa wakulima

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:391
  • Today's page views 393
  • Total visitors 20,702
  • Total page views 23,076

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In