• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, October 12, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

ACT Wazalendo waeleza wanafunzi vyuo vikuu walivyokosa udahili,mikopo fani ya udaktari,famasia

Wapo pia walioomba radiolojia na teknolojia ya viumbe hai

by bajeti
October 11, 2026
in Sayansi na Teknolojia
0
ACT Wazalendo waeleza wanafunzi vyuo vikuu walivyokosa udahili,mikopo fani ya udaktari,famasia

Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Chama cha ACT Wazalendo Riziki Mngwali

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema kimepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wanaotaka kusoma udaktari na famasia katika vyuo vikuu mbalimbali nchini wakilalamikia kukosa udahili kwa awamu ya kwanza na ya pili.

Mbali na wanafunzi wanaotaka kusoma udaktari na famasia lakini pia wapo walioomba radiolojia na teknolojia ya viumbe hai ni miongoni mwa wanaolalamikia ugumu wa kupata nafasi.

Akizungumza na waaandishi wa habari mkoani Dar es Salaam Oktoba 11,2026, Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Riziki Shahani Mngwali amesema wamepokea malalamiko ya wanafunzi wengi walioomba masomo ya udaktari kwa zaidi ya vyuo vitano na kukosa vyote, licha ya kuwa na vigezo.

Amesema wameona taarifa ya Tume ya Vyuo vikuu (TCU) ya Oktoba 3, 2026 kuhusu kuongeza muda kwa waomba udahili kwa awamu ya tatu.

“Kila mwaka, kumekuwa na wanafunzi wengi wanaokosa kuendelea na masomo licha ya kufaulu masomo yao kutokana na ugumu wa taratibu za udahili kwenye baadhi ya vyuo vikuu”

“Wanafunzi wanaotaka kusoma udaktari, famasia, radiolojia na teknolojia ya viumbe hai ni miongoni mwa wanaolalamikia ugumu wa kupata nafasi”

“Baadhi yao wameomba katika vyuo vingi na kulipa ada za maombi mara kadhaa bila kupata udahili, hali inayoongeza gharama kwa familia na kuhatarisha ndoto zao za kitaaluma”amesema Mngwali

Mngwali amebainisha kuwa kutokana na uchache wa nafasi za masomo katika vyuo na wanafunzi wengi wanaomaliza katika masomo hayo inaleta adha kwao na kupoteza fedha za maombi bila mafanikio.

“Wanafunzi wengi wamekosa udahili kwa awamu mbili katika vyuo vifuatavyo;Kairuki,KCMC,Rabininsia, St. Joseph,Kampala University (KIU)  Bugando, Muhimbili , UDSM, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA)”amesema Mngwali

Hata hivyo Mngwali ameongeza kuwa  kukosa kwa nafasi katika masomo ya sayansi na udaktari inawalazimu wanafunzi wengi kuomba taaluma za sayansi ya jamii (Social sciences) ambapo wapo wanafunzi wengi wanaokosa kuanza vyuo kwa sababu za changamoto za udahili.

 “ACT Wazalendo, tunaitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu nchini wanapata haki hiyo.

“Asitokee mwananfunzi mwenye sifa kukosa chuo na Serikali pia iongeze uwekezaji katika miundombinu, wakufunzi na vifaa vya mafunzo ili kupanua nafasi za masomo, hususan katika fani muhimu kwa maendeleo ya taifa”amefafanuwa Mngwali

Akizungumzia kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa nyuo vikuu,Mngwali ameeleza kuwa ACT Wazalendo, wamebaini kuwa mfumo wa sasa wa ugharamiaji wa elimu ya juu kwa sehemu kubwa unategemea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) lakini unaendelea kuacha wasiwasi wa uwezo wake wa kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na uhitaji wanapata ufadhili wa kutosha.

Amesema ACT Wazalendo wamebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya wanafunzi wataokosa mikopo au kupangiwa fedha zisizokidhi mahitaji yao kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambapo kwa mwaka wa masomo 2026/2027, hadi Agosti 31, 2026, waombaji walikuwa 157,309.

Hata hivyo, katika awamu ya kwanza iliyotangazwa jana Oktoba 10, wanafunzi 84,180 pekee ndio wamefanikiwa kupata mikopo, huku wanafunzi 73,129 wamekosa mikopo hiyo.

Mngwali amehusisha mwenendo huo kuwa  unawakumbusha mwaka wa masomo wa 2025/26 ambapo takwimu zinaonesha kuwa Bodi ya Mikopo ilipokea maombi 150,530 na kupanga mikopo kwa wanafunzi 106,606, huku waombaji 43,924 wakikosa kabisa.

Amesema mwaka huu tayari Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb), aliliambia Bunge kupitia hotuba ya bajeti kuwa Serikali imepanga kutoa mikopo kwa wanafunzi wapya 111,692.

Amesema kila mwaka, mfumo wa mikopo ya elimu ya juu umekuwa ukikabiliwa na changamoto za upangaji, ambapo baadhi ya wanafunzi hukosa mikopo kabisa na wengine hupangiwa fedha zisizotosheleza mahitaji yao, ikiwemo mikopo ya kujikimu pekee au asilimia ndogo ya ada.

“Hali hii huwalazimisha baadhi kuacha masomo, kusoma katika mazingira magumu, kupoteza umakini au kufanya shughuli za kiuchumi ili kujikimu, huku wengine wakitumia fedha za kujikimu kulipia ada.

“Wazazi na walezi nao hulazimika kuuza mali na rasilimali zao kugharamia elimu, licha ya changamoto za upatikanaji wa ajira, hali inayozidisha umasikini katika familia”amesema Mngwali

Mngwali amesema ACT Wazalendo wanaona kuwa mfumo huo unawanyima maelfu ya wanafunzi wenye uhitaji fursa ya elimu, unakatisha ndoto za watoto wa familia maskini na kufilisi rasilimali za familia.

“Kwa msingi huo, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora na bure kuanzia elimu ya awali hadi shahada ya kwanza.

“Serikali ichukue wajibu wa kugharamia elimu ya umma badala ya kuhamishia mzigo kwa wazazi na kuwaingiza wanafunzi katika madeni.

“Tunaitaka ifute mfumo wa mikopo kwa ajili ya ada, utafiti na mahitaji ya kimasomo, na badala yake ilipe gharama hizo kwa wanafunzi wote waliodahiliwa katika vyuo vikuu na vyuo vya kati na HESLB ibaki kutoa mikopo ya kujikimu kwa ajili ya chakula na malazi”amesema Mngwali

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 22,464
  • Total page views 25,035

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In