• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, October 14, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Prof.Hamad aonya uharibifu wa mazingira Kisiwa cha Uzi,Zanzibar

by bajeti
October 13, 2026
in Mazingira
0
Prof.Hamad aonya uharibifu wa mazingira Kisiwa cha Uzi,Zanzibar

Mnadhimu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Omar Fakih Hamad (wa kwanza kulia) akiangalia moja ya eneo linalochimbwa mchanga katika Kijiji cha Uzi Kisiwani kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja,Zanzibar wakati alipotembelea kisiwa hicho Oktoba 13,2026.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR

MNADHIMU Mkuu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Omar Fakih Hamad,ameitaka Serikali kuiangalia kwa karibu hali ya Kisiwa cha Uzi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja akisisitiza umuhimu wake katika uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii.

Prof.Hamad amehimiza umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja ili kulinda fukwe, mikoko, miti ya asili na rasilimali nyingine zinazokifanya kisiwa hicho kuwa na thamani ya kipekee.

Prof.Hamad ameyasema hayo Oktoba 13, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili wananchi katika kisiwa hicho ambapo shughuli za uchimbaji mchanga na ukataji wa miti zikielezwa kushamiri.

Amesema ni muhimu kwa  wananchi pia  kushirikiana katika kukiendeleza kisiwa chao na kulinda rasilimali zilizopo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Aidha amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya jamii unaweza kuleta madhara makubwa kwa wakazi wote wa kisiwa hicho.

“Kwa sababu wachimbaji wa mchanga na wanaokata miti ya asili wanatoka humu humu Uzi, nawaombeni sana mshirikiane kuulinda urithi wenu ambao ni muhimu kwa Taifa,”

“Madhara ya uharibifu wa mazingira yatawakumba kwanza wananchi wa Uzi wenyewe, hivyo  ni  kuna umuhimu wa kuchukua hatua za pamoja kulinda fukwe, mikoko, miti ya asili na rasilimali nyingine zinazokifanya kisiwa hicho kuwa na thamani ya kipekee”amesema Prof. Hamad

Mnadhimu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Omar Fakih Hamad (wa kwanza kulia) akiangalia moja ya eneo linalochimbwa mchanga katika Kijiji cha Uzi Kisiwani kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja,Zanzibar wakati alipotembelea kisiwa hicho Oktoba 13,2026.

Wakizungumzia hali ya uharibifu wa mazingira katika Kijiji cha Uzi Kiswani baadhi ya wananchi  wameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika maeneo ya fukwe za bahari kisiwani humo, wakieleza kuwa shughuli hiyo inatishia usalama wa makazi yao na mustakabali wa kisiwa hicho.

Mmoja wa wananchi wa kisiwa hicho Omar Suleiman amesema uchimbaji wa mchanga katika fukwe za bahari umewaingiza hofu kubwa kutokana na kuongezeka kwa hatari ya maji ya bahari kufika katika makazi yao.

“Kwa kweli hii ni dalili ya kupoteza kisiwa, kwani maji ya bahari kila uchao yanakuja majumbani kwetu kutokana na uchimbaji wa mchanga ufukweni,” amesema Suleiman.

Naye Mahadhi Abdulkheiry amesema Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kukomesha uchimbaji wa mchanga, akionya kuwa kutokuchukua hatua kunaweza kusababisha kisiwa cha Uzi kutoweka kutokana na athari za kimazingira.

“Kila unapopita, iwe ufukweni au kwenye makazi yetu, utaona mashimo ya kila aina ambayo yametuongezea hatari kwa watoto wetu na hata sisi wazee,” amebainisha  Abdulkheiry.

 

Mnadhimu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Omar Fakih Hamad (katikati) akimsikiliza mkazi wa Kisiwa cha Uzi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja,Zanzibar wakati alipotembelea kisiwa hicho Oktoba 13,2026.

Kwa upande wake  Marhumi Hemed Suleiman ameongeza kuwa hali ya uchimbaji wa mchanga inatia wasiwasi kuhusu usalama wa kisiwa hicho na maisha ya wananchi, akitaka hatua za haraka zichukuliwe kabla madhara hayajawa makubwa zaidi.

Mbali na uchimbaji wa mchanga, wananchi hao wameitaka Serikali kupiga marufuku uvuvi unaotumia nyavu zinazoharibu mazingira ya baharini, wakieleza kuwa unachangia uharibifu wa matumbawe na samaki wachanga.

Mselemu Ali Fumu alisema uvuvi huo una madhara makubwa kwa viumbe wa baharini na kuathiri mazingira ambayo wananchi wanayategemea kwa shughuli zao za kiuchumi.

Kisiwa cha Uzi ni miongoni mwa visiwa vidogo vya Zanzibar ambavyo vimeendelea kuhifadhi uasili wake, vikionesha utajiri wa mazingira ya asili, mandhari ya kuvutia.

Next Post
Makamu wa Rais Ndejembi aiagiza TANESCO kupeleka transfoma ya megawati 50 Katavi ifikapo Desemba mosi.

Makamu wa Rais Ndejembi aiagiza TANESCO kupeleka transfoma ya megawati 50 Katavi ifikapo Desemba mosi.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 22,491
  • Total page views 25,065

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In