• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, October 14, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Makamu wa Rais Ndejembi aiagiza TANESCO kupeleka transfoma ya megawati 50 Katavi ifikapo Desemba mosi.

Mkurugenzi wa TANESCO aahidi kukamilisha

by bajeti
October 13, 2026
in Habari
0
Makamu wa Rais Ndejembi aiagiza TANESCO kupeleka transfoma ya megawati 50 Katavi ifikapo Desemba mosi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Deogratius Ndejembi akiwasalimia wananchi wa Mpanda, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi, akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2026 na Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 13,2026.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KATAVI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi,ameagiza kuharakishwa kwa miradi ya barabara, maji na umeme mkoani Katavi, huku akiwataka wakandarasi wanaosuasua kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi waanze kunufaika na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali.

Maagizo hayo ameyatoa Oktoba 13,2026 wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda, akiwa njiani kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, ambapo alipata fursa ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akicheza ngoma ya kabila la wafipa, wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi, akielekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2026 na Kumbukizi ya Miaka 27 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 13, 2026.

Akizungumzia changamoto ya umeme, Makamu wa Rais amelitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha hadi kufikia Desemba 01, 2026, Mpanda inapelekewa Transfoma itakayoongeza megawati 50 zaidi za umeme ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezeka katika Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya mkoa huo.

Makamu wa Rais amesisitiza kuhakikisha ahadi ya kukamilisha maboresho hayo inatekelezwa, sambamba na kuweka nguzo za zege.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameonesha kutoridhishwa na kusuasua kwa ujenzi wa barabara za lami zenye thamani ya Sh. Bilioni 29, akitaka kujua sababu za kuchelewa kwa kazi licha ya wakandarasi kuwa katika maeneo ya miradi.

Ameagiza mitambo kuingizwa kazini mara moja, huku akitaka hatua za haraka zichukuliwe katika barabara ya kuelekea Kigoma, hususani eneo la Mtonyamasi ambako ujenzi wa daraja na sehemu nyingine za barabara haujakamilika, hususani kwenye kipindi hiki ambacho kumekuwa na tahadhari kubwa ya mvua za El-nino.

Pia ameelekeza kuharakishwa kwa ujenzi wa kilomita 20 za barabara inayoelekea Bandari ya Karema, akisisitiza umuhimu wa barabara hiyo katika kufungua fursa za biashara, usafirishaji na kukuza uchumi wa Katavi.

Makamu wa Rais amesisitiza matarajio ya Serikali ni kuona kazi zinakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa.

Akitoa maelezo, Mkurugenzi wa TANESCO   Lazaro Twange, kuhusu mpango wa kuongeza uwezo wa umeme hadi megawati 80,ameahidi kufikia tarehe 01 Desemba miundombinu ya kuongeza umeme Mpanda itakuwa imekamilika na kutatua changamoto kubwa ya upungufu wa umeme iliyopo sasa mkoani Katavi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amempongeza Makamu wa Rais kwa kuwasili mkoani humo na kumwomba kufikisha salamu za shukrani kwa Rais kutokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali uliofanyika Katavi,

Amesema zaidi ya Sh.Trilioni 1.4 zimeelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma za wananchi na kukuza uchumi wa mkoa huo.

Makamu wa Rais amewasali mkoani Katavi akiwa njiani kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa kumwakilisha Rais katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2026 akiwa  ameambatana na Waziri wa Maji  Jumaa Aweso.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 22,491
  • Total page views 25,065

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In