• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

UN yataka mapambano mabadiliko tabianchi

by BAJETI
May 31, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

SEOUL,Korea Kusini

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema  dunia inahitaji ushirikiano wa kimataifa kushinda janga la ugonjwa wa Corona  ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Akizungumza kupitia  ujumbe wa video katika  ufunguzi wa mkutano wa ushirikiano wa kimataifa wa mwaka 2021 wa P4G unaofanyika mjini Seoul chini Jamhuri ya Korea Kusini  amesema ikiwa serikali zitaafikiana kwa pamoja malengo ya kumaliza makaa ya mawe, kuongeza ahadi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuwekeza katika malengo ya dunia, kuna fursa ya kuishinda  mabadiliko ya tabiachi.

Amesema   dunia inahitaji ushirikiano wa kimataifa kushinda janga la Corona kufikia Malengo ya maendeleo  ya maendeleo endelevu na kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo wa ushirikiano wa ukuaji unaojali mazingira na malengo ya Ulimwengu 2030 (P4G) unakusudia kukuza ushirikiano wa soko na kuchagiza hatua za ngazi ya juu za kisiasa na sekta binafsi na umewajumuisha pamoja wakuu wa nchi, wakurugenzi watendaji na viongozi wa asasi za kiraia karibu na ajenda ya pamoja ya kuhamasisha uwekezaji kwa ajili ya mabadiliko yanayoonekana.

Akizungumzia kuhusu hewa ukaa, Guterres ameelezea kwamba  ingawa kuna ahadi za kufanikisha kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo 2050, bado kuna  mengi ya kufanya ili kuziba pengo la uzalishaji wa hewa ukaa na kufikia malengo ya SDGs.”

Amesisitiza wito wake kwa wafadhili wote kuwasilisha michango mipya waliyoamua Kitaifa, kujitolea kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050 na muhimu zaidi  wa kuweka sera na mipango kuelekea kufikia lengo hilo.

Aidha amebainisha kuwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi uso kwa uso kutasaidia kuwalinda watu walio katika mazingira magumu zaidi  wakati wa kujikwamu kutoka klwenye janga la Corona( COVID-19) na kipaumbele cha kwanza sasa hivi ni kuweka mipango na sera kuzuia mitambo mipya ya makaa yam awe na kuacha matumizi ya makaa ya mawe ifikapo mwaka 2040. 

Ameongeza kuwa “nchi zilizoendelea bado hazijatimiza ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 kwa juhudi za hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kusaidia jamii zilizo katika mazingira magumu ambazo tayari zinateseka na athari za ongezeko la joto duniani.”

Amefafanua kuwa mtu mmoja kati ya watatu ulimwenguni bado hawajafanikiwa  vya kutosha na mifumo ya tahadhari ya mapema, ambapo wanawake na wasichana, ambao ndio asilimia 80 ya wale wanaolazimika kuhama kutokana na dharura ya mabadiliko ya tabianchi, bado mara nyingi hutengwa na maamuzi ya kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

mwisho

Next Post

Waandishi wa Mazingira

Waandishi watakiwa kuandika habari za mazingira

Matumizi ya baiskeli yanahifadhi mazingira

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In