• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

Kuachiwa Uamsho uwe mwanzo kutendewa haki mahabusu

by BAJETI
November 22, 2021
in Makala
0
Kuachiwa Uamsho uwe mwanzo kutendewa haki mahabusu
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

TAASISI ya Hizb ut Tahrir Tanzania imesema kuachiwa huru kwa masheikh wa Uamsho uwe mwanzo wa kutendewa haki kwa mahabusu wengine waliobakia gerezani.

Kauli ya taasisi hiyo ya kidini imekuja siku chache baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)Sylvester Mwakitalu kuwafutia mashitaka yaliyokuwa yanawakabili masheikh wa Uamsho ikiwemo ya ugaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari  kutoka Hizb ut Tahrir Tanzania Masoud Msellem amesema uhuru wa Uamsho uwe mwanzo wa kutendewa haki mahabusu wengi waliobakia kwa kuwa baadhi ya sheria zinatumika vibaya.

Amesema kufutwa mashtaka ya Uamsho ni hatua muhimu ya kutia moyo, lakini huo uwe mwanzo tu wa safari ndefu kwa taasisi za kusimamia haki kwa kwenda mbali zaidi, kwa kuwa kuna mahabusu wengi wa mashtaka kama hayo ya ugaidi.

Amesema  kwa mfano ndani ya Dar es Salaam pekee kabla ya kuachiwa Uamsho kulikuwa na mahabusu wa aina hiyo wengi pamoja na Arusha  na Tanga.

“Ndani ya Mtwara kuna wenzetu watatu wa Hizb ut Tahrir Tanzania,  Ustadh Ramadhani Moshi Kakoso , Omar Salum Bumbona Waziri Mkaliaganda ambao nao wamekuwa mahabusu kwa mashtaka kama hayo ya ‘ugaidi’kwa karibu miaka minne sasa”amesema Msellem.

Msellem amebainisha kuwa baada ya Uamsho kukaa mahabusu kwa miaka saba kwa tuhuma za ugaidi, hatima ya mashtaka hayo imewapa sura ya kuwepo utamaduni wa dhulma na uonevu ikiwemo kesi za kubambikiza kwa wasio na hatia kupitia mgongo wa sheria ya ugaidi, kama ambavyo pia inavyolalamikiwa  sheria ya uhujumu uchumi.

Aidha amefafanua kuwa  wao kama Hizb ut Tahrir Tanzania wanaendelea  kusisitiza msimamo wao juu ya taasisi zinazosimamia haki kutekeleza majukumu yao kwa kusimamia haki.

“Mahabusu wote katika mikoa mbalimbali waachiwe huru, wapewe dhamana au kesi zao zisikilizwe kwa haraka na katika hilo tunavitaka vyombo vyote vya kusimamia haki vijizatiti katika majukumu yao hayo kwa weledi, uaminifu na haki kama alivyosema Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ka”amesema Msellem

MWISHO

Next Post

NCMC:Pandeni miti kukabiliana na hewa ukaa

Othman arejea Zanzibar

UN:Shughuli za ujenzi huchangia asilimia 39 uchafuzi wa hewa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In