• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

UN:Shughuli za ujenzi huchangia asilimia 39 uchafuzi wa hewa

by BAJETI
June 24, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

MAJENGO  pamoja na  shughuli za ujenzi  huchangia asilimia 39 ya hewa chafuzi ya ukaa duniani.

Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha miji kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira duniani (UNEP) Marino Otto.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Otto amesema kiwango hicho kinajumuisha hewa chafuzi zitokazo kwenye majengo mathalani kupitia hewa itolewa nje na viyoyozi pamoja na malighafi zitumikazo kujenga majengo hayo.

Amesema  majengo yaliyojengwa kwa saruji na vyuma  huchangia asilimia 11 ya uchafuzi wa mazingira.

“Viwanda vya saruji vinatarajiwa kuzalisha hewa chafuzi ya ukaa asilimia tano ambayo itachochea kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi kama sekta moja. Sekta hiyo kwa kugundua changamoto hiyo inajizatiti kupunguza uchafuzi, lakini hiyo bado haitoshi.”amesema Otto

Otto amesema mbadala wa ujenzi ambao unajali mazingira ni ule unaotumia mbao ambazo amesema

“Tani moja ya saruji inatoa tani moja ya hewa ya ukaa wakati ikitengenezwa, na tani moja ya mbao kupitia miti ambako inatolewa inasaidia kuondoa tani mbili za hewa ya ukaa kutoka kwa mazingira.”

Ameongeza kuwa ni muhimu kuwa na usimamizi endelevu wa  misitu kwa kuhakikisha kuwa kila mti unaokatwa mwingine unapandwa ili kuzingatia ulinzi na  uhifadhi wa mazingira katika nyanja tofauti.

Katika juhudi za kupambana na hali hiyo,Serikali nchini Tanzania iliamua kuanzisha Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Kaboni(NCMC) kupitia Chuo cha Misitu,Wanyama Pori na Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Akizungumzia umuhimu wa Kituo hicho na mabadiliko ya tabia nchi,Mkurugenzi wa NCMC Prof.Eliakim Zahabu amesema kazi kubwa ya kituo hicho ni kuratibu upimaji,uwasilishwaji na uhakiki wa takwimu za kaboni (hewa ukaa) kwa niaba ya serikali.

“Miti hutengeneza chakula chake kwa kufyonza hewa ukaa na kutoa hewa ya oksijeni na wakati huo huo kaboni inahifadhiwa kwenye miti,hivyo basi kukua kwa miti kunatokana na kiwango cha kaboni kilichohifadhiwa kwenye mti”amesema Prof.Zahabu

MWISHO

Next Post

EWURA yakabidhi mashuka 43I kusaidia vituo vya afya Dodoma

Mabadiliko hali ya hewa kuhamisha watu milioni 10 Bangladesh

Joto kali lasababisha shule kufungwa Canada

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In