WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje wa Bangladesh Abul Kalam Abdul Momen amesema kwamba idadi ya raia wa nchi wanaopaswa kuhamishwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa imezidi milioni 10.
Momen ameyasema hayo jana kwenye mpango wa hali ya hewa ulioandaliwa na Tume Kuu ya Bangladesh na Baraza la Hamlet Tower huko London, mji mkuu wa Uingereza, kupitia mkutano wa video.
Shirika la Habari la TRT la nchini Uturuki limemnukuu Momen akieleza kuwa nchi yake tayari imekaribisha wakimbizi Waislamu Milioni 1.1 wa Rohingya kutoka nchini Mynamar.
Amesema zaidi ya watu milioni 10 wa nchi hiyo ambao wanapaswa kuhama kwa sababu zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Momen pia amefafanua kuwa wale ambao walipaswa kuhama kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa kama wanajulikana kama “wakimbizi wa hali ya hewa” ambapo nchi yake ni moja ya wahanga wa ongezeko la kiwango cha joto duniani,
Momen ameongeza kuwa ifikapo mwaka 2050, kuongezeka kwa kiwango cha bahari kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa kunaweza kufurika kwa asilimia 17 ya pwani ya Bangladesh, na hali hiyo inaweza kuwaondoa zaidi ya watu milioni 20.
Discussion about this post