• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Joto kali lasababisha shule kufungwa Canada

by BAJETI
June 30, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

CANADA imekumbwa na joto kali linalofikia nyuzi joto 46.1 hali iliyosababisha migahawa, maduka  na shule kufungwa katika baadhi ya maeneo.

Mbali na kufungwa kwa shule na shughuli zingine za kijamii theluji pia imeyeyuka na kusababisha kuongezeka kwa kina cha maji ya mto, hali iliyopeleka wananchi kuhamishwa.

Wimbi hilo la joto, limeathiri zaidi magharibi mwa nchi hiyo, limesababisha msimu wa joto mkali zaidi katika miaka 84 iliyopita nchini humo.

Kulingana na Huduma ya Hali ya Hewa ya Canada, joto la nyuzi 46.1 lililorekodiwa katika jimbo la British Columbia juzi alasiri na kurekodiwa kama joto la juu kabisa kuwahi kutokea nchini humo.

Rekodi ya awali ya joto la juu katika historia ya nchi hiyo ilikuwa nyuzi 45 Celsius, iliyorekodiwa katika jimbo la Saskatchewan mnamo Julai 1937.

Wakati joto hilo likiongezeka,imeripotiwa kuwa theluji iliyeyuka haraka zaidi ya inavyotarajiwa kwa sababu ya joto hilo, ambapo nyumba nyingi zimehamishwa kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji katika mto.

Mtaalam wa hali ya hewa katika Wizara ya Mazingira ya hiyo  Derek Lee,    ,amekielezea chombo cha habari cha  CBC kuwa joto litapanda zaidi kutoka nyuzi 46.1 hadi kuweza kufikia nyuzi joto  50 za Celsius katika maeneo mengine.

Kwa upande mwingine, vituo vya kupoza joto vimefunguliwa katika baadhi ya maeneo mengi kati miji ya nchi hiyo dhidi ya athari mbaya za hali ya hewa ya joto.

Haya hivyo kliniki ambazo zinatoa chanjo ya ugonjwa wa corona(COVID-19) zimeamua kuahirisha kazi zake.

Kuongezeka kwa viwango vya joto duniani kunasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi hasa uchafuzi wa hali ya hewa.

Moja ya athari mbaya zaidi za ongezeko la joto ni kuibuka kwa moto katika maeneo mbali mbali ya misitu duniani hali inayopelekea maelfu ya watu kuhamishwa ambapo moja kati ya nchi  inayoathirika  sana na ongezeko la joto ni Australia.

Athari za mabadiliko ya tabia nchi zimeendelea kuiathiri dunia kwa kuongezeka viwango vya joto kali huku baadhi ya miji ikitabiriwa kuzama kutokana na ongezeko la kina cha maji baada ya theluji kuyeyuka.

Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO) umeulelezea mwaka 2019 kama mwaka uliokuwa na joto kali zaidi duniani baaya ya mwaka 2016

MWISHO

Next Post

Ufugaji nyuki husaidia utunzaji wa mazingira

TAWA:Chatu ndiye nyoka mkubwa pekee asiye na sumu

Pikipiki zapigwa marufuku Afghanistan

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In