• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Ufugaji nyuki husaidia utunzaji wa mazingira

by BAJETI
July 1, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema sekta ya ufugaji nyuki ina mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii,kiuchumi na uhifadhi wa mazingira nchini..

Mbali na hilo lakini pia sekta ya ufugaji nyuki huboresha uhifadhi wa bioanuwai ambapo kupungua na kutoweka kwa nyuki wa asali kunaweza kutumika kama kiashirio cha kuharibika kwa mazingira.

Hayo yamo katika Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki iliyoandaliwa na wizara hiyo ambayo imetolewa leo mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’ ili kuwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.

Sera hiyo imefafanua kuwa licha ya kutoa mchango mkubwa wa uhifadhi wa mazingira lakini pia ufugaji nyuki ni chanzo cha chakula (asali),malighafi kwa ajili ya viwanda(mishumaa ya nta,vipodozi,nguo na mafuta ya kulainishia ),madawa na mapato kwa wafugaji nyuki.

Sera hiyo imeeleza kuwa ukadiriaji wa athari kwa mazingira ni chombo kitumikacho kusaidia katika utoaji wa maamuzi ili kuhakikisha kwamba hasara na uharibifu wa mazingira unaepukwa.

“Lengo la jumla  la Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ni kuongeza mchango wa sekta hii kwa maendeleo endelevu ya Tanzania, na kuboresha uhifadhi na usimamizi wa maliasili yake kwa  manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho”imeeleza sera hiyo.

Sera hiyo imebainisha kuwa inakadiriwa  uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini Tanzania unaweza kufikia takribani tani 138,000 za asali na tani 9,200 za nta kwa mwaka kutokana na makundi makubwa ya nyuki yanayokadiriwa  kuwa milioni 9.2.

“Ufugaji wa nyuki ambao ni stadi na sayansi ya utunzaji wa nyuki wa asali unatoa mchango mkubwa  katika kuboresha bioanuai hasa nyuki wa asali ambao hujumuisha wale waumao(Apis mellifera spp) na wale wasiouma(Trigoma au Melipona spp).

“Usimamizi wa mazingira ni jukumu la kila mtu ambapo majukumu makubwa ya taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ni kuisaidia jamii kwa kuwapa mwamko kuhusu hali yao na kuwaunga mkono ili wawajibike”imefafanua sera hiyo

Next Post

TAWA:Chatu ndiye nyoka mkubwa pekee asiye na sumu

Pikipiki zapigwa marufuku Afghanistan

Mfuko wa Misitu wawezesha miradi zaidi ya 500 kuboresha maisha ya wananchi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In