• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, April 30, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

EWURA yakabidhi mashuka 43I kusaidia vituo vya afya Dodoma

by BAJETI
June 24, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imetoa msaada wa mashuka 431 yenye thamani ya Sh.Milioni tano kwa vituo vinne vya afya vilivyopo jijini  Dodoma ili kusaidia uboreshaji wa huduma za afya’

 hilo ambalo linakabiliwa na ongezeko la idadi ya watu.

Akizungumza mara bada ya kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa EWURA, Mhandisi Godfrey Chibulunje,amesema kuwa wametoa msaada huo ili kuongeza kasi ya utoaji huduma za afya kwa wananchi kupitia vituo vya afya vinne ambavyo ni Makole, Mkonze, Hombolo na Kikombo.

Mhandisi Chibulunje amesema Jiji la Dodoma ni kati ya majiji yayaokuwa kwa kasi na kuongeza idadi ya watu hivyo msaada huo wameutoa ikiwa ni mchango wa mamlaka hiyo   kwa jamii hususan katika kipindi hiki cha kuhitimisha wiki ya utumishi wa umma nchini .

Amesema kuwa  msaada huo utasambazwa katika vituo vya afya vilivyolengwa kwa kuzingatia mahitaji halisi katika kila kituo.

“Tumetoa msaada wa mashuka 431 kwa Jiji la Dodoma na yataenda kwa vituo vinne cha Makole, Hombolo, Mkonze na Kikombo na sisi mwaka huu  tumechagua  eneo la afya ili kusaidia jamii”amesema Mhandisi Chibulunje.

Mhandisi Chibulunje ameongeza kuwa katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma, mamlaka hiyo imetoa mafunzo kwa watumishi wake na kutembelea watoa huduma mbalimbali wanaowasimamia kubaini changamoto wanazokabiliana nazo ili waweze kuzitatua kwa kuwa lengo lao ni kuhakikisha mlaji anapata huduma bora kwa viwango vinavyosimamiwa na mamlaka yao.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dk. Andrew Method,amesema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa na kwamba wanaishukuru EWURA kwa  msaada huo

Amesema  wanaishukuru EWURA kwa kuendelea kusaidia sekta ya afya katika  jiji hilo ambapo tayari ilikwishatoa msaada wa vifaa vya kutunza watoto njiti

 Dk.Method amesema kwa mwezi katika Kituo cha Afya cha Makole wajawazito wanaojifungua  ni zaidi ya 400 ambapo  kwa wastani , wajawazito 120 wanajifungua kila wiki.

mwisho

Next Post

Mabadiliko hali ya hewa kuhamisha watu milioni 10 Bangladesh

Joto kali lasababisha shule kufungwa Canada

Ufugaji nyuki husaidia utunzaji wa mazingira

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:16
  • Today's page views 18
  • Total visitors 16,001
  • Total page views 18,157

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In