• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

NCMC:Pandeni miti kukabiliana na hewa ukaa

by BAJETI
June 22, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

RIPOTI ya Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO) imeonesha kuwa kuna ongezeko zaidi la hewa chafuzi katika anga  

Ripoti hiyo iliyotolewa Novemba 25, 2019 mjini Geneva nchini Uswisi ilieleza kuwa  hali hiyo inayoendelea kwa muda mrefu inamaanisha kuwa vizazi vijavyo vitakabiliana na ongezeko la matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ongezeko la joto, mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, upungufu wa maji, kuongezeka kwa kina cha bahari na uharibifu kwa viumbe wa majini na ardhini.

Katika taarifa hiyo ya WMO kuhusu hewa chafuzi ilionesha kuwa viwango vya wastani vya hewa ya ukaa (CO2) viliongezeka na kufikia kufikia 407.8 kwa 1,000,000 mwaka 2018 ikilinganishwa na kutoka 405.5 kwa 1,000,000 mwaka 2017.

Kwa  mujibu wa taarifa hiyo,ongezeko la hewa ukaa yaani CO2 kutoka mwaka 2017 hadi 2018 lilikuwa karibu sawa na lile lililoshuhudiwa kuanzia mwaka 2016 hadi 2017 na juu kiasi ya wastani kwa muongo mmoja uliopita.

Viwango vya kimataifa vya CO2 vilipita kiwango cha juu cha 400 kwa 1,000,000 katika mwaka 2015.

Hata hivyo wataalamu wanaeeleza kuwa hewa ukaa inasalia katika anga kwa karne kadhaa.

Akizungumza juu ya ripoti hiyo Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema hakuna dalili ya kupungua kwa mkusanyiko wa hewa chafuzi katika anga licha ya ahadi zote za mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Amesema wanahitaji kutafsiri ahadi hizo kwa vitendo na kuongeza kiwango cha matamanio kwa ajili ya ustawi wa baadaye wa jamii.

Hata hivyo Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoathirika na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha  na mrundikano wa gesi joto angani(hewa ukaa)

Gesi joto hizo zinatokana na shughuli za binadamu kama vile viwanda,magari,nishati na ukataji wa misitu.

Hata hivyo hewa ukaa ndio gesi joto iliyoko angani kwa kiasi kikubwa  ambapo ni misitu pekee ndiyo yenye uwezo wa kusafisha hewa hiyo.

Katika juhudi za kupambana na hali hiyo,Serikali iliamua kuanzisha Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Kaboni(NCMC) kupitia Chuo cha Misitu,Wanyama Pori na Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Akizungumzia umuhimu wa Kituo hicho na mabadiliko ya tabia nchi,Mkurugenzi wa NCMC Prof.Eliakim Zahabu anasema kazi kubwa ya kituo hicho ni kuratibu upimaji,uwasilishwaji na uhakiki wa takwimu za kaboni kwa niaba ya serikali.

Anasema majukumu mengine ni pamoja na kuhusisha sekta nyingine zinazozalisha hewa joto na kutoa ushauri wa namna upimaji,uwasilishaji na kuhakiki takwimu ili kulinda maslahi ya jamii na mazingira.

“kazi nyingine ya kituo ni kutoa ushauri wa kisera na kisheria na kutengeneza ripoti na machapisho yanayohusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mfumo wa kitaifa wa takwimu za kaboni.

“Miti hutengeneza chakula chake kwa kufyonza hewa ukaa na kutoa hewa ya oksijeni na wakati huo huo kaboni inahifadhiwa kwenye miti,hivyo basi kukua kwa miti kunatokana na kiwango cha kaboni kilichohifadhiwa kwenye mti”anasema Prof.Zahabu

Prof.Zahabu anafafanua kuwa kupanda misitu mipya na kutunza misitu ya asili  ni njia zinazokubalika katika jitihada za kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi duniani.

“Nchi ,mashirika na watu binafsi wenye kuwajibika na usafi wa mazingira wanawajibu wa kupunguza viwango vya  hewa  mkaa wanavyozalisha na njia wanazoweza kutumia kupunguza uzalishaji wa hewa mkaa ni kuboresha nishati wanazotumia wenyewe na kufadhili shughuli za upandaji na utunzaji wa misitu kwenye nchi za kitropiki”anasema Prof.Zahabu

Akizungumzia kuhusu soko la kaboni,Prof.Zahabu anabainisha kuwa Soko rasmi la Kaboni ni kwa kupitia Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Mabadiliko  ya Hali ya Hewa  duniani (UNFCC)  hususani Sera ya Maendeleo  safi(CDM) ya Protokali  ya Kyoto ambayo inaruhusu shughuli za upandaji wa miti mipya na kwa Tanzania mikoa inayofanya miradi ya Kaboni ni Mbeya,Katavi na Arusha”

“Shughuli zingine kama utunzaji shirikishi wa misitu ya jamii (CFM) nchini unaohusisha misitu asilia ambayo ingetoweka ama kuharibika na kutoa hewa ukaa(Kaboni) inaweza pia kupata malipo kupitia Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na ukataji  miti hovyo na uharibifu wa misitu”

“Ukiona mti umekuwa ujue umehifadhi kiwango kikubwa cha Kaboni na ukichoma misitu basi ujue kaboni inakwenda angani na kwa Tanzania matumizi ya kilimo ndio yameonekana kuzalisha Kaboni kwa wingi kutokana na watu kufyeka misitu na kuchoma moto ili kuandaa mashamba”anasema Prof.Zahabu

Kwa upande wake Mkuu wa  Chuo cha Misitu,Wanyamapori na Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)Prof. Suzana Augustino anasema Tanzania ni nchi mwanachama wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuthibiti mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) ulioanzishwa mwaka 1992.

Anasema mpango huu unatoa wito kwa nchi wanachama kupunguza Gesi Joto (GHGs) katika anga ambazo ndizo sababu ya mabadiliko ya tabianchi.

“Athari za mabadiliko tabianchi ni pamoja na kuongezeka kwa ukame na mafuriko ya mara kwa mara, uhaba wa chakula na maji, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama Malaria na Homa ya Bonde la Ufa (RVF), kuyeyuka kwa seruji kwenye milima mirefu na kwenye ncha za Dunia na vile vile kutoweka kwa visiwa vidogo”anasema Prof.Augustino

Aidha anafafanua kuwa kuna juhudi za kitaifa na kimataifa za kushughulikia mabadiliko ya Tabianchi na  mojawapo ni  ni biashara ya kaboni (hewa ukaa).

Anabainisha kuwa biashara ya kaboni ya misitu ilikuwa inawezekana tu kupitia sera ya maendeleo safi (CDM) ya Itifaki ya Kyoto ya UNFCCC ambapo shughuli za upandaji miti mipya zinaruhusiwa.

 “Mtu akiona misitu ajue ameona hela na mtu anatunza miti ili kupata fedha  hivyo hii nayo ni fursa ya kuuza Kaboni na ndio maana serikali iliamua kuanzisha pia Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Kaboni(NCMC)”anasema Prof.Augustino.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUA Dkt.Deo Shirima anasema kila kitu kinachofanyika lazima kichangie asilimia kadhaa ya fedha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa hata ukipanda ndege unachangia pia hewa ukaa.

Anasema badhi ya nchi tayari wameweka viwango vya kuchangia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuweka asilimia kadhaa za fedha katika tiketi za ndege ili kuchangia kwa kuwa matumizi ya kila siku ya binadamu ikiwemo kutumia magari,ndege,viwanda na mengine huchangia ongezeko la gesi joto na matokeo yake ni kuona athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) John Chikomo anasema wao kama wadau wa mazingira wamekuwa wakihakikisha kuwa vyombo vya habari nchini kupitia waandishi wao vinajikita katika kuandika taarifa za mazingira.

“Tumeshawapeleka waandishi wa habari kujifunza mambo ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo  Thailand,Uganda,Ghana ili kujifunza zaidi  habari za mazingira na athari zake”anasema Chikomo

Chikomo anabainisha kuwa ni wajibu wa JET kuisaidia serikali katika kupambana na masuala ya mazingira hasa mabadiliko ya tabia nchi ili kusaidia kizazi cha sasa na kijacho kwa faida ya Taifa.

“JET itaendelea kuhakikisha kuwa wandishi wa habari wanajikita zaidi katika kuandika habari za mazingira ili kusaidia nchi kwa vizazi vya sasa na vijavyo na kulinda mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu”anasema Chikomo

MWISHO

Next Post

Othman arejea Zanzibar

UN:Shughuli za ujenzi huchangia asilimia 39 uchafuzi wa hewa

EWURA yakabidhi mashuka 43I kusaidia vituo vya afya Dodoma

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In