MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amerejea nyumbani kisiwani Zanzibar leo Juni 23, 2021 akitokea jijini Dar es Salaam.
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais alikuwa jijini Dar es Salaam alikokuwa kwa shughuli maalum za kichama tangu Juni 19, 2021.
Akiwa jijini Dar es Salaam, Othman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo alihudhuria kikao cha Kamati kuu pamoja na kufanya ziara ya kuwajulia hali wagonjwa na wananchi wenye matatizo mbali mbali.
Mbali na hilo lakini pia amezungumza na wanachama na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa, Jimbo na Kata ya Mbagala Kuu.
mwisho
Discussion about this post