• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TGDC: Megawati 5000 nishati ya jotoardhi hazijaendelezwa

by BAJETI
July 2, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

TANZANIA inakadiriwa kuwa na hifadhi zaidi ya megawati 5000 za nishati ya jotoardhi ambazo hazijaendelezwa hadi kufikia sasa na kuanza kutumika.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo mkoani Dar es Salaam na Kampuni ya Uendelezaji  Jotoardhi Tanzania (TGDC) katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’

TGDC ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) chini ya Wizara ya Nishati na ilianzishwa ili kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme  wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali ambapo serikali iliamua kuwa na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme vya nishati jadidifu ikiwemo jua,upepo na jotoardhi.

Taarifa hiyo ya TGDC imefafanua kuwa mpaka sasa kuna maeneo zaidi ya 52 yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi kutokana na tafiti za awali za kisayansi.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopo katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki  na kujaliwa kuwa na rasilimali nyingi za nishati za jotoardhi na kukadiliwa kuwa na zaidi ya megawati 5000 na hii inaashiria kuwa Tanzania ina hifadhi kubwa ya nishati jotoardhi”imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa aina hiyo ya nishati ni ya uhakika,safi(haichafui mazingira) na ni endelevu ambapo hadi 2018 TGDC imefanya tafiti katika maeneo ya Songwe,Ngozi-Mbeya,Luhoi-Pwani,Kisaki-Morogoro,Natron-Arusha,Ibadakuli-Shinyanga na Mbaya Kiejo-Mbeya.

“Nishati ya jotoardhi ni nishati inayotokana na joto linalotoka katika miamba joto ambalo ni kali na halina ukomo hivyo huchemsha maji ya mvua yanayoingia ardhini kupitia mpasuko mbalimbali katika uso wa dunia”imeongeza taarifa hiyo.

TGDC imeongeza ni lazima mvuke unaotokana na maji hayo ya moto ufikie nyuzi joto 107 hasi nyuzi joto 300 ndipo umeme unaweza kuzalishwa kwa kutumia mitambo maalum ya kufua umeme(Turbine) ambalo huzungushwa na mvuke unaotoka ardhini kwa mgangamizo  mkubwa.

Hata hivyo TGDC imebainisha kuwa mbali na kuzalisha umeme lakini pia maji hayo ya moto kutoka chini ya ardhi yanaweza kutumika kupasha moto mitambo viwandani,kupasha moto nyumba,vitalu kwa ajili ya kilimo,kukausha mazao ya kilimo.

Kazi nyingine ya jotoardhi ni pamoja na kupasha moto kwenye mabwawa ya kufugia samaki  na ya kuogelea,shughuli za utalii,hutumika kama tiba,kupoza na kugandisha.

Nishati hiyo ya jotoardhi ni maji ya moto yanayotoka chini ya ardhi ambapo baadhi ya maeneo hutumika kama sehemu za kitamaduni kwa wananchi kuchemshia vyakula jamii ya mizizi kama viazi,mihogo na kisha kuoga maji hayo ili kuondoa mikosi.

Next Post

Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere kujazwa maji ifikapo Novemba

TGDC kuanza kuchoronga visima nishati jotoardhi

Mahakama Inayotembea kupelekwa mikoa mingine kwa awamu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:25
  • Today's page views 25
  • Total visitors 13,182
  • Total page views 14,928

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In