• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TGDC kuanza kuchoronga visima nishati jotoardhi

by BAJETI
July 4, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

KAMPUNI ya Uendelezaji  Jotoardhi Tanzania (TGDC) imesema inatarajia kuchoronga visima vitatu vya utafiti na uhakiki wa nishati ya jotoardhi(majimoto) nchini.

TGDC ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) chini ya Wizara ya Nishati ilianzishwa Desemba 2013 ili kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme  wa kutosha kutokana na sababu mbalimbali ambapo serikali iliamua kuwa na vyanzo vingine vya uzalishaji wa umeme vya nishati jadidifu ikiwemo jua,upepo na jotoardhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TGDC mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’ imesema kuwa maeneo saba waliyafanyia utafiti na uhakiki wa kisayansi lakini matatu kati ya hayo ndiyo watachoronga visima.

Taarifa hiyo ya TGDC imefafanua kuwa mpaka sasa kuna maeneo zaidi ya 52 yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi (maji ya moto) yanayotoka chini ya ardhi kutokana na tafiti za awali za kisayansi.

Aidha taarifa hiyo imeongeza  kuwa hadi kufikia mwaka 2018 TGDC ilikuwa imefanya tafiti zaidi kwenye maeneo ya Songwe-Songwe,Ngozi-Mbeya,Mbaka Kiejo-Mbeya,Luhoi-Pwani,Ibadakuli-Shinyanga,Kisaki-Morogoro na Natron-Arusha

“Lakini hadi kufikia Januari 2019 maeno yaliyokuwa yamefakwisha fanyiwa tafiti na yalikuwa kwa uchorongaji wa visima vya utafiti na uhakiki wa nishati ya jotordhi ni  Ngozi mkoani Mbeya,Mbaka Kiejo mkoani Mbeya pia  na Songwe mkoani Songwe”imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa baada ya uchorongaji visima vya utafiti na uhakiki ,hatua itakayofuata ni uchongaji visima vya uzalishaji.

Taarifa hiyo ilifafanua pia kuhusu Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo linauhusiano wa moja kwa moja na nishati ya jotoardhi kutokana na kwamba lina viashiria vya chemichemi za majimoto  chini ya Ziwa hilo pamoja na kemikali zinazopatika katika maji yake.

“Asili ya Ziwa Ngozi inatokana na mlipuko wa volkano ambayo kisayansi ina uhusiano wa moja kwa na nishati ya jotoardhi ambapo vielelezo vya kisayansi vinafafanua kuwa nishati ya joto ardhi inatokana na joto asilia linalozalishwa katikakati ya tabaka au kitovu cha duani”imeeleza taarifa hiyo.

Next Post

Mahakama Inayotembea kupelekwa mikoa mingine kwa awamu

PURA:Uzalishaji wa gesi asilia wafikia futi za ujazo Bilioni 5.4

EWURA CCC:Mtumiaji wa huduma za nishati na maji ana haki ya kufidiwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:3
  • Today's page views 3
  • Total visitors 16,270
  • Total page views 18,443

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In