• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, May 12, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

EWURA CCC:Mtumiaji wa huduma za nishati na maji ana haki ya kufidiwa

by BAJETI
July 5, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji ((EWURA CCC) limesema mtumiaji wa huduma hizo ana haki ya kufidiwa kutokana na kupatiwa huduma mbovu kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo.

Baraza hilo ambalo limeanzishwa chini ya kifungu namba 30 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ya mwaka 2001,Sura ya 414 lina dhamira ya kutetea haki za watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa kukuza ufahamu kwa umma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza hilo leo mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’

EWURA CCC imesema kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2021 Baraza hilo imewafikia zaidi ya watumiaji 4200 wa huduma hizo ambapo  malalamiko 800  yametatuliwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtumiaji wa huduma hizo ana haki ya utatuzi mzuri wa madai  yake kama hasara imetokana na mtoa huduma.

Aidha imeongeza kuwa mtumiaji wa huduma hizo pia ana haki ya kuelimishwa kuhusu huduma zitolewazo ili kumpa maarifa na ujuzi kumwezesha kuchagua huduma stahiki.

“Haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma hizi ni pamoja na haki ya kufidiwa ,haki ya utatuzi mzuri wa madai,kufidiwa kutokana na kupatiwa bidhaa zenye dosari au huduma mbovu na madai yote ya fidia yazingatie kanuni na taratibu zilizopo”Imefafanua taarifa hiyo.

Mbali na hilo lakini pia mtumiaji wa huduma hizo ana haki na wajibu wa usalama na faragha,kupata taarifa,kuchagua huduma,kusikilizwa, kuwakilishwa na kuwa katika mazingira bora.

“Wajibu wa mtumiaji ni kulipa ankara kwa wakati kwa mujibu wa kanuni,taratibu na viwango vilivyowekwa,kutoa taarifa,kutunza miundombinu na matumizi halali ya miundombinu”imebainisha taarifa hiyo

Next Post

TANESCO yaeleza faida za mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere(JNHPP)

TMDA:Kunusa na kuweka ugoro mdomoni ni kosa kisheria.

Mradi wa Julius Nyerere umezalisha ajira zaidi ya 7400

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 16,174
  • Total page views 18,341

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In