• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mradi wa Julius Nyerere umezalisha ajira zaidi ya 7400

by BAJETI
July 6, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere(JNHPP)  kwa kutumia maji ya Mto Rufiji  umetoa ajira zaidi ya 7400 huku watanzania wakipewa kipaumbele.

Mradi  huo ambao utapelekea kupatikana kwa bwawa la nne kwa ukubwa barani Afrika linatarajia  kuzalisha megawati 2115 za umeme ifikapo mwaka 2022.

Akizungumza leo mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’,Mhandisi wa Shirika hilo Mwanji Mhaka amesema hadi kufikia mwezi Mei,2021 mradi huo ulikuwa na wafanyakazi zaidi ya 7400.

Amesema kati ya hao asilimia 89.09 ni watanzania na wageni ni asilimia 10.91 ambapo wanawake ni zaidi ya 270 waliopata ajira katika mradi huo.

“Kwa sasa mradi upo kwenye kilele ambapo hadi kufikia Mei 2021 ujenzi wa bwawa hilo ulifikia asilimia 52 na kazi iliyobaki sasa ni kufunga mashine na kazi nyingine ndogondogo hivyo wafanyakazi wataendelea kupungua wakati mradi unaelekea kukamilika kwa kuwa kazi nyingi zitakuwa zimekamilika ”amesema Mhandisi Mhaka

Mhaka amebainisha kuwa wafanyakazi watapungua kwa kuwa kazi nyingi zitamalizika na zilizobaki ni za kufunga mashine ambapo ifikapo Novemba 15,2021 wataanza kujaza maji katika bwawa hilo.

Akizungumzia kuhusu faida  zitakazopatikana kwa upande wa vijiji vinavyozunguka bwawa hilo,Mhaka ameeleza kuwa baada ya umeme kuanza kuzalishwa vijiji hivyo vitafaidika na ujenzi wa huduma za kijamii.

“Vijiji vitajengewa Hospitali,Shule,Visima vya Maji,Vituo vya Polisi na ujenzi wa barabara  na gharama za umeme zitapungua zaidi”amesema Mhaka

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa barabara zinazoelekea katika mradi huo,Mhaka amefafanua kuwa kipande cha barabara kinachoanzia eneo Fuga hadi ndani ya mradi kitajengwa kwa lami na barabara inayopita Ubena  Zomozi,Ngerengere,Mvua,Kisaki hadi eneo la mradi zitaimarishwa zaidi.

“Barabara ya Kibiti,Mloka hadi eneo la mradi nayo itajengwa ili kuhakikisha kuwa inapitika wakati wote”amesema Mhandisi Mhaka

Next Post

TANESCO:Mradi wa JNHPP unalinda mazingira.

Mzumbe yawezesha vijana kujiajiri

Baba Mtakatifu ateuwa maaskofu Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 13,276
  • Total page views 15,024

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In