SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere(JNHPP) kwa kutumia maji ya Mto Rufiji unalinda mazingira kwa asilimia 100.
Bwawa hilo ambalo ni la nne kwa ukubwa barani Afrika linatarajia kuzalisha megawati 2115 za umeme ifikapo mwaka 2022.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa bwawa hilo leo katika mkoani Dar es Salaam Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’Mhandisi wa TANESCO Mwanji Mhaka amesema suala la uharibifu wa mazingira ni la kufikirika katika mradi mradi huo.
Amesema eneo la Selous lina ukubwa wa kilomita za mraba 55,000 lakini ujenzi wa mradi huo ni asilimia 1.92 pekee za eneo hilo.
Amesema si kwamba eneo hilo limechimbwa lote ili kutengeneza bwawa bali kinakachofanyika ni kuyazuia maji ya Mto Rufiji ambayo yatarudi nyuma kilomita 100 na kisha kutengeneza bwawa hilo.
“Suala la uharibifu wa mazingira ni la kufikirika kwa kuwa ni sehemu ndogo sana ya eneo la Selou ndio linatumika katika ujenzi hivyo suala hilo ni kitua ambacho hakipo”amesema Mhaka
Mhaka amefafanua kuwa mradi huo pia utatunza zaidi mazingira kwa kuwa utadhibiti mafuriko katika baadhi ya vijiji kama Ikwiriri na Mtanza na vingine vingi kutokana na maji yake kuwa katika mtitiriko maalum pindi ujenzi wa mradi huo utakapokamila na kuanza kuzalisha umeme.
“Kutakuwa na maeneo ya wanyama wanaoishi majini kuendelea na maisha yao kama kawaida lakini pia kuna mitambo ambayo itakuwa inasafisha kama kuondoa mizoga ya wanyama na vitu vingine.
“Chini ya bwawa kumejengwa mfumo ambao kama kuna tope basi linaweza kuondolewa kwa kuwa maji yanayopita chini yana nguvu kubwa hivyo kuna vipimo vya kuonesha suala hilo na mitambo itaruhusu maji kupita kwa chini ili yaondoe tope hilo kutokana na nguvu ya maji”amesema Mhaka
Mradi huo unajengwa na Kampuni ya Arab Contractors kwa kushirikiana na Elsewelde kutoka nchini Misri ambapo unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 15,2022.
Discussion about this post