MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa tahadhari kwa watumiaji wa kunusu na kuweka mdomoni bidhaa za tumbaku ukiwemo ugoro kuwa ni kosa kisheria.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya TMDA ilitolewa leo mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’
TMDA imeeleza kuwa ni kosa kisheria kutafuna kunusu na kuweka mdomoni bidhaa za tumbaku.
TMDA ambayo ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ina jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti usalama,ubora na ufanisi wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi nchini.
“Uthibiti wa Tumbaku,Je wajua kuwa kutafuna,kunusa na kuweka mdomoni bidhaa za tumbaku kama vile ugoro ni kosa kisheria”imeeleza taarifa hiyo.
Uthibiti wa matumizi ya bidhaa hizo umekuja wakati ambapo makundi ya vijana yakionekana kuwa ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hizo hasa ugoro ambao miaka ya nyuma ulitumika sana kwa watu wenye umri mkubwa (wazee).
Hata hivyo mapambano ya TMDA katika kukabiliana na suala hilo yanatokana na dhima ya taasisi hiyo kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula,dawa vipodozi na vifaa tiba.
Discussion about this post