• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

PURA:Uzalishaji wa gesi asilia wafikia futi za ujazo Bilioni 5.4

by BAJETI
July 5, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema hadi kufikia mwezi Januari mwaka huu uzalishaji wa gesi asilia nchini ulikuwa futi za ujazo Bilioni 5.4 .

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo mkoani Dar es Salaam katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba yenye kauli mbiu ‘ Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu’

PURA imesema uzalishaji wa gesi asilia katika visima vya Mnazi Bay kwa mwezi Januari 2021 ulikuwa wastani wa futi za ujazo Bilioni 2.39 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo Milioni 74 kwa siku.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa kwa upande wa uzalishaji wa gesi asilia katika visima vya Songo Songo ulikuwa wastani wa futi za ujazo Bilioni 3.038 kwa mwezi  ambapo ni sawa na futi za ujazo Milioni 98 kwa siku.

“Hadi kufikia mwezi Januari 2021,jumla ya  uzalishaji wa gesi asilia umefikia wastani wa futi za ujazo Bilioni 5.428 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo Milioni 172 kwa siku”ilifafanua taarifa hiyo

PURA ambayo iko chini ya Wizara ya Nishati imeundwa kupitia kifungu namba 11 cha Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, imeanzishwa kufuatia ongezeko la ugunduzi wa gesi asilia nchini na kubadilishwa kwa sheria ya Petroli.

“Dhima ya PURA ni kuthibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli kwa uwazi,weledi na ufanisi ili kuchangia katika ustawi wa jamii na kiuchumi kwa watanzania”imeeleza taarifa hiyo.

Hata hivyo PURA ina malengo ya kuimarisha ushiriki wa wazawa na manunuzi ya bidhaa na huduma za wazawa katika tasnia ya bidhaa za petroli.

Mbali na hilo lakini pia wanamelengo ya kuimarisha uwekezaji katika mkondo wa juu wa petroli na kuhakikisha kuwa mgao wa serikali unaongezeka.

“Majukumu ya PURA ni pamoja na kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu mkondo wa juu wa petroli,kusimamia na kudhibiti shughuli za mkodo wa juu wa petroli na kusimamia shughuli zote za miradi ya kusindika gesi asilia kwa kimiminika”imeongeza taarifa hiyo.

Next Post

EWURA CCC:Mtumiaji wa huduma za nishati na maji ana haki ya kufidiwa

TANESCO yaeleza faida za mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere(JNHPP)

TMDA:Kunusa na kuweka ugoro mdomoni ni kosa kisheria.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In