• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, April 28, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Rais mstaafu ataka kujinyonga

by BAJETI
August 22, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

LA PAZ,BOLIVIA

RAIS  wa zamani wa mpito wa Bolivia Jeanine Anez amefanya jaribio la kujiua akiwa mahabusu  siku moja baada ya kufunguliwa mashtaka ya “mauaji ya halaiki”

Rais huyo wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi hiyo, amefunguliwa mashitaka  kutokana na vifo vya waandamanaji vilivyotokea mwaka 2019.

Wakili wa Anez, Jorge Valda, amesema kiongozi huyo wa zamani ambaye amefadhaishwa na tuhuma zinazomkabili alijaribu kujiua lakini jaribio hilo lilishindwa.

Anez, amekuwa gerezani  tangu mwezi Machi mwaka huu kwa madai ya kufanya mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake na rais wa zamani wa Bolivia, Evo Morales.

Anez aliingia madarakani kama kiongozi wa mpito mwaka 2019 baada ya Morales kujiuzulu na kuikimbia nchi hiyo lakini wapinzani wanasema hatua yake ya kuchukua madaraka ilikuwa sawa na mapinduzi.

Hata hivyo Disemba 31,2019, serikali yake iliamua kuwafukuza mabalozi wa ngazi za juu wa Mexico na Uhispania, baada ya jaribio la maafisa wa serikali ya zamani kuondoka kwenye ubalozi wa Mexico kwa msaada ya balozi wa Uhispania na kutoroka nchi.

Rais huyo mstaafu alisema kuwa Balozi Maria Teresa Mercado wa Uhispania na afisa wa ubalozi huyo anayehusika na usalama hawatakiwi kuwapo Bolivia ndani ya masaa 72 yajayo. 

Uhispania nayo iliwafukuza maafisa watatu wa ubalozi wa Bolivia kujibu hatua hiyo. 

Maafisa tisa wa serikali ya Rais Evo Morales iliyopinduliwa kufuatia maandamano ya umma na uingiliaji kati kijeshi, ambao waliomba hifadhi kwenye ubalozi wa Mexico.

Serikali ya mpito ya Bolivia iliwafungulia mashitaka maafisa hao wakiwatuhumu kwa uchochezi, ugaidi na wizi wa kura, na imewakatalia kutoka nje ya nchi.

Januari 25,2020 ,serikali ya Rais Anez, ilivunja  mahusiano ya kidiplomasia na Cuba na kuwarudisha nyumbani watoa huduma za afya kutoka Cuba zaidi ya 700 waliokuwa nchini humo.

Machi 13,2021 Anez,alizuiliwa kwa mashtaka ya ugaidi,ghasia na njama ndani ya upeo wa uchunguzi unaojulikana kama “kesi ya mapinduzi”.

Kulingana na habari ya gazeti la Elpais, serikali ya Bolivia ilitangaza kuwa Anez, ambaye hati ya kukamatwa kwake ilitolewa, alikuwa akizuiliwa katika eneo la Trinidad mkoani Beni.

Kama sehemu ya uchunguzi, hati ya kukamatwa ilitolewa kwa Anez, Waziri wa zamani wa Serikali Arturo Murillo, Waziri wa zamani wa Utawala Yerko Nunez, Waziri wa zamani wa Sheria Alvaro Coimbra, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa zamani Luis Fernando Lopez na Waziri wa zamani wa Nishati Rodrigo Guzman.

Ilitangazwa kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa sababu ya uwezekano wa maafisa wa serikali wa zamani wanaotuhumiwa kwa ugaidi, uasi na njama ya kutoroka nchini na kuzuia mchakato wa uchunguzi.

Kufuatia hati ya kukamatwa, Coimbra na Guzman walizuiliwa katika mkoa wa Beni nchini humo kama sehemu ya uchunguzi, ambao Rais wa zamani Evo Morales aliuelezea kama “mapinduzi” na akachunguza sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake, na kusema kuwa mawaziri hao wawili wangehamishiwa mji Mkuu wa La Paz.

Kwa upande mwingine, Anez, alichapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya hati ya kukamatwa, na kudai kwamba chama tawala kiliamua kurudi kwenye udikteta, kwa kutumia “mateso ya kisiasa na dhuluma.

Novemba 13,2020 Anez ambaye alikuwa makamu wa pili wa Rais wa Bunge la Seneti alijitangaza kuwa rais wa mpito wa Bolivia, licha ya kukosekana kwa idadi ya wabunge inayohitajika, akisema ameamua hivvo kutokana na kwamba kuna ” umuhimu wa kuweka mazingira sawa ya amani ya kijamii”.

Muda mfupi baada ya Anez kujingaza rais wa mpito,Morales alijibu kwa kusema kuwa jaribio la mapinduzi la kushangaza na la aibu katika historia ya Bolivia limefanyika.

Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales akiwasili nchini Mexico muda mfupi baada ya kuikimbia nchi yake Novemba 12,2019(Picha na mtandao)

Amesema Seneta kutoka mrengo wa kulia uliofanya jaribio la mapinduzi amejitangaza kuwa rais wa Seneti, kisha kaimu rais wa Bolivia bila idadi inayohitajika ya wabunge kupasisha tangazo lake, huku akizungukwa na kundi lililohusika katika jaribio hilo la mapinduzi na kuongozwa na jeshi na polisi wanaokandamiza raia.

Next Post

Aliyepata chanjo ya COVID-19 kutambuliwa kimataifa

Sh.Bilioni 1.5 kuanza kutatua kero ya mafuriko Malinyi

Akamatwa akipeleka mahari ukweni

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:28
  • Today's page views 37
  • Total visitors 15,961
  • Total page views 18,111

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In