• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, December 5, 2025
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Tanzania ina nguruwe milioni 3.2

by BAJETI
August 24, 2021
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

TANZANIA ina nguruwe wanaofikia milioni 3.2 wanaofugwa na wakulima mbalimbali nchini ambapo upande wa Zanzibar wanyama hao wamefikia 2,209.

Hayo ni kwa mujibu wa  Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 katika Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki iliyotolewa Agosti mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Katika Sensa hiyo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa kilimo 2019/20 ilihusisha aina mbalimbali za mifugo inayofugwa nchini.

Aidha aina kuu za mifugo iliyoainishwa katika taarifa hiyo ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe na kuku.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Matokeo Muhimu kwa Sekta za mazao,mifugo na ufugaji wa samaki, taarifa kuhusu idadi ya mifugo zilikusanywa Agosti mosi, 2020, na taarifa nyingine za mifugo zilikusanywa kwa kufuata mwaka wa kilimo wa 2019/20.

Katika ripoti hiyo maalum,matokeo hayo ya Sensa yanaonesha kuwa, idadi ya nguruwe ni 3,208,495, kwa upande wa wakulima wadogo Tanzania Bara wanyama hao walikuwa 3,201,163 na upande wa Zanzibar kwa wakulima wadogo walikuwa ni 2,209

Kwa upande wa mashamba makubwa wanyama hao walikuwa ni 5,123 kwa  Tanzania Bara na upande wa Zanzibar walikuwa sifuri.

“Ujumbe muhimu wa Sensa hiyo ni kwamba idadi ya mifugo imekuwa ikiongezeka katika vipindi vitatu vya Sensa (2002/03, 2007/08 na 2019/20).

“Uhusiano wa Kisera, ongezeko la idadi ya mifugo linaweza kuwa limechangiwa na sera inayolenga kuongeza uzalishaji wa mifugo wa kibiashara ili kuweza kufikia viwango vya masoko ya ndani na nje, kuongeza kipato cha wafugaji na kuboresha hali ya maisha ya wafugaji.

“Ongezeko la idadi ya mifugo haliakisi mchango wa sekta hii kwenye Pato la Taifa ambao umeendelea kubakia chini ya asilimia mbili”ilibainisha ripoti hiyo.

Next Post

Rais Durtete kugombea kama makamu wa rais 2022.

Walimu kuchanjwa kwa lazima chanjo ya UVIKO-19

Fukwe za Dar es Salaam kuwa za kitalii

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 12,059
  • Total page views 13,712

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In