WAKATI nchi nyingi duniani zikitoa uhuru kwa wananchi wake kuamua kuchanjwa au kutochanjwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19,Marekani imewata wafanyakazi wote katika shule za umma jijini New York kuchanjwa ifikapo Septemba 27,mwaka huu.
Marekani imetoa kauli hiyo mara baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchi hiyo (FDA) kutoa idhini kamili ya dawa aina ya Pfizer / BioNTech kama chanjo ya UVIKO-19,
Meya wa Jiji la New York Bill de Blasio alitangaza kuwa kila mtu anayefanya kazi katika shule za umma lazima awe na kipimo cha kwanza cha chanjo ifikapo Septemba 27.
Awali, wafanyakazi wa shule za umma jijini humo walilazimika kuchanjwa au kupimwa mara kwa mara, kama wafanyakazi wengine wa jiji.
Wanafunzi milioni moja katika Jiji la New York wataanza shule mnamo Septemba 13.
Discussion about this post